Saladi Ya Bilingani Tango, Vitunguu Vyeupe Na Parsley

Saladi Ya Bilingani Tango,  Vitunguu Vyeupe Na Parsley

Vipimo na Namna ya Kutayarisha

Bilingani ndogo ndogo freshi Osha, katakata vipande vya mraba (cubes) - 5

Majani ya saladi (lettuce) Osha, katakata - 2 majani

Tango Osha, katakata - 2

Vitunguu vyepe Menya, katakata - 2

Nyanya/tungule Osha, katakata - 1

Parsley majani Osha, chuja maji, katakata - 1 mshikano (bunch)

Siki - 2 vijiko vya supu

Chumvi – Kisia

Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia bilingani - kiasi

Namna Ya Kutayarisha:

  1. Weka mafuta kiasi katika karai, wash moto.
  2. Kaanga bilingani katika mafuta yamoto, zikiiva na kugeuka rangi epua weka katika chujio zichuje mafuta.
  3. Katika bakuli, tia vitu vyote isipokuwa chumvi na siki.
  4. Karibu na kula, changanya vitu vyote utie chumvi na siki, uchanganye vizuri.

Majani ya parsley:

 

 

 

 

Share