Saladi Ya Komamanga Pilipili Boga Tango

Saladi Ya Komamanga Pilipili Boga Tango

Vipimo na Namna ya Kutayarisha

Majani ya saladi (lettuce) osha chuja maji - 1 msongo (bunch)

Komamanga chambua  - 2

Pilipili boga (Capsicum) la kijani osha katakata vipande kwa urefu kama picha – 1

Pilipili boga la rangi ya manjano – 1

Pilipili boga la rangi ya orengi – 1

Matango osha, katakata vipande virefu refu - 2

Namna Ya Kutayarisha:

  1. Katika bakuli jengne changanya vitu vyote isipokuwa majani ya saladi. Bakisha kidogo chembe za komamanga.
  2. Chukua bakuli jengine la kuweka mezani, panga majani ya saladi pembezoni.
  3. Weka mchanganyiko wa pilipili boga, tango na komamanga  katikati ya bakuli.
  4. Mwagia komamanga zilobakia upambe vizuri ikiwa tayari kuliwa

 

 

 

 

Share