Steki Ya Ng’ombe Na Mifupa Ya B.B.Q (T-Bone Steak)

 Steki Ya Ng’ombe Na Mifupa Ya  B.B.Q (T-Bone Steak) 

  

Vipimo  

Nyama ya T-Bone Steak - 15 Ratili (LB) 

Pilipili mbichi - 5 

Tangawizi mbichi - 1 

Kitunguu saumu (thomu/galic)  - 1 Uwa/msongo (bunch) 

Jiyra/Cummin (bizari ya pilau)  - 1 kijiko cha supu 

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha supu 

*Sosi ya B.B.Q  - 1 kikombe   

Kilainisho cha nyama (meat tenderizer) - 1 kijiko cha chai 

Ndimu  - ¼ kikombe 

Chumvi - kiasi 

Mafuta ya kupakiapakia wakati wa kuchoma   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Safisha nyama acha ichuje maji yote. 
  2. Menya tangawizi mbichi, kitunguu thomu, kisha weka katika mashine ya kusagia pamoja na pilipili mbichi, chumvi, ndimu  saga mpaka ilainike 
  3. Mimina katika bakuli kisha changanya na pilipili ya unga, jiyra, kilainisho cha chama  na sosi ya B.B.Q ya tayari. 
  4. Changanya pamoja na nyama kisha ifunike vizuri weka katika friji irowane kwa muda wa masaa 4 au zaidi. 
  5. Koleza chumvi na ikihitajika.  
  6. Choma katika makaa au jiko la B.B.Q huku unageuzageuza na kupakaza mafuta hadi iwive. 

Kidokezo:  

1-Ukikos sosi ya B.B.Q inayouzwa tayari madukani, tayarisha  Sosi ya ukwaju inayopatikana katika kiungo kifuatacho: 

Sosi Ya Ukwaju  

2- Nzuri kutolewa na mikate ya Pita Pan au Naan  na  sosi ya hummus   inayopatikana katika kiungo kifuatacho 

Hummus (Shaam)

  

 

                                                                                                                  

 

                            

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share