Ghiybah Inaweza Kuwa Moyoni?

SWALI:

 

Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh, Sheikh suali langu ni hili wakati mwengine ndani ya moyo wangu hufikiri ghyiba lkn ndani ya nafsi yangu sisengenyi na mtu je hii ni ghyba au

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kama ghiybah kama inaweza kuwa moyoni.

Ghiybah ni ‘amali na kitendo cha moyo ndio Ma-Imaam wengi wa Hadiyth kama vile Imaam an-Nawawiy wana mlango wa Kuharamisha Kusikiliza Ghiybah na Uharamu wa Ghiybah.

 

Tatizo lako ni huenda ikawa ni kuwa kilichoko moyoni mwako na kutekelezwa na ulimi na hivyo huenda ukaingia katika ghiybah na upate madhambi kwa hilo la kutoka kwenye kinywa. Allaah Aliyetukuka Anasema yafuatayo kuhusu uharamu wa ghiybah na kuuhifadhi ulimi:

Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu” (al-Hujurat [49]: 12).

 

Na Allaah Anatukataza na kusikiliza ghiybah, Anasema kutupa maelekezo endapo tutasikia:

Na wanaposikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na nyinyi mna vitendo vyenu. Salaamun ‘Alaykum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki kujibizana na wajinga” (al-Qaswasw [28]: 55).

 

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate manufaa zaidi:

 

Madhara Ghiybah - An-Namiymah  

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share