Afuturu Jua Linapozama Au Afuate Ratiba Waliyopewa Japokuwa Jua Halijazama Kabisa?

SWALI:

 

asalam alykum, mimi ni muslimu na nafunga ramadhani hila nipo BELGIUM hivyo inaniwia ugumu kujua muda sahii wa kufungua mana navyofahamu mimi unaweza kufungua pale jua linapozama ila sisi huku maeneo ninapohishi tumepewa ratiba jinsi swala ya magharibi inapoinia ni saa 2 nadakika 45 hivyo ni muda muufaka wa kufukulia ila jua bado linakuwa alijazama kabisa, hivyo naomba ufafanuzi kuhusu swala hili.

   

 WABILLAH TAWFIQ


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu wakati wa kufungua.

Hakika inavyotakikana ni kutazama jua na si kutegemea ratiba za Msikitini ila tu isipokuwa jua halionekani kutokana na mawingu na sababu zingine. Na ikiwa ni kufuata ratiba basi iwe ni ratiba inayoendana sambamba na mawio.

 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ya Imaam al-Bukhaariy na Muslim alimuagiza Swahaba ateremke kwenye kipando na kuwatayarishia chakula cha wao kufungua. Yule Swahaba ilimshangaza kwani alikuwa anaona bado mwangaza wa jua, hivyo akasita kidogo. Na hapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Jua linapozama upande wa Magharibi na kiza kutokeza upande wa Mashariki basi huwa amefungua aliyefunga.

 

Kwa hiyo, huo mwangaza usikusumbue maadam hizo ndizo nyakati za watu wa huko za kuingia Magharibi na Swalaah yake. Na maadam Mashaykh wa huko wameshayakinisha kuwa Magharibi imeingia watu waliofunga wanatakiwa wafanye haraka kufungua.

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Inafaa Kufuturu Wakati Wekundu Bado Haujamalizika?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share