Wakristo Wanafunga Na Kuswali Pamoja Na Waislamu

SWALI:

ASALAMU ALAIKUM
Ndugu zangu waislam naomba mtusaidie kwa hili swali sisi vijana tunafanya kazi katika camp ya oil desert (machimboni) wakati wa ramadhani kuna kikosi cha wazungu wanataka kufunga. Na wao sio waislam na hawajatawariwawako jamaa wana sema ina faaa Wanawaleta mpaka imefika wanasali na sisi je ndugu zangu vipi hukmu yake Na kweli inafaa hawa jamaa waingie mskitini.  

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Tunamuhimidi Allah ambaye ametupatia neema nyingi na Yeye pekee ndiye wa kushukuriwa.

  Swali hili la ndugu zetu ni zuri na hapa ndio tunaona umuhimu wa Da‘wah (kuwalingania wasiokuwa Waislamu) kwa njia iliyo nzuri, mawaidha mazuri na hekima ya hali ya juu. AlhamduliLlaah, hawa ni watu ambao wamejileta wenyewe katika Msikiti. Na asiyekuwa Muislamu anaweza kuingia katika Msikiti kama alivyofanya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kuwaruhusu Wakristo wa Najran kuingia na kujadiliana nao na kuwaacha hata kulala ndani. Kuhusu kufunga ni hiari yao kwani Ummah hata zilizotangulia ziliamrishwa na Allah kufunga hivyo katika hilo hatuwezi kuwaingilia isipokuwa kwa kufanya hivyo hawatakuwa ni wenye kupata thawabu yoyote kwani kusihi Swalah na funga ni kutekeleza nguzo zake na misingi yake ya kukubaliwa mikubwa ni:

1.    Ikhlasi.

2.    Kufuata alivyofanya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)

Hivyo, nasaha yetu ni kuwa waacheni wafanye hayo lakini nanyi mzungumze nao kwa njia iliyo nzuri ili muwalete katika Dini yetu.

Na Allah Anajua zaidi 

 

 

Share