Amefiwa Na Ndugu Yake Akiwa Mbali, Anaweza Kumswalia Swalaatul-Ghayb?

 

Amefiwa Na Ndugu Yake Akiwa Mbali, Anaweza Kumswalia Swalaatul-Ghayb?

 

Alhidaaya.com

 

  

Swali:

  

Ndugu yangu kafa lakini mimi sinipo naweza kumsaliya mahali nilipo?

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakika ni kuwa mtu hafai kumswalia yeyote yule aliyekufa mbali ikiwa maiti ataswaliwa na Waislamu waliopo huko. Itafaa kwako kumswalia hapo ulipo ikiwa huko alikofia nduguyo hakuna Waislamu na hivyo hakuswaliwa. 

 

Kwa sasa ni vigumu kupata sehemu ambayo hakuna Waislamu. Kitu ambacho unaweza kufanya ni kumuombea du’aa kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amghufurie na Amrehemu. 

 

Soma jibu kuhusiana na swali kama lako katika kiungo kifuatacho:

 

Swalaah Ya Ghayb (Kumswalia Swalaah Maiti Aliye Mbali)

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share