Kusafirisha Maiti Japo Kuna Waislamu, Kuipeleka Alipotoka Inajuzu?

SWALI:

 

ASSALAM alykum wa -RAHMA tuh wa barakatuh. MWENYEZI MUNGU akujaliyeni kila la kheri na afya njema. Nina shukuru kwa msaada wenu na kwakujitolea kutu elimisha.

 

Swali langu nikuomba kuelimishwa mimi na wenzangu kuhusu maisha tunao kwa wakazi wa europa. Je, ni halali kusafirisha maiti, ikiwa kuna waislam hapo?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kuisafirisha maiti ili kwenda kuizika sehemu nyingine.

Haijapatikana kabisa katika historia na maisha ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi  wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) kuwa walisafirisha maiti ili kwenda kuzikwa sehemu nyingine.

 

Hivyo, haijuzu kwa Muislamu kusafirisha maiti ya Muislamu kuipeleka sehemu nyingine ili ipate kuzikwa. Ni jukumu la Waislamu wa sehemu hiyo kumfanyia mambo manne maiti huyo, nayo ni:

 

1.   Kumuosha.

 

2.   Kumkafini.

 

3.   Kumswalia.

 

4.   Kumzika.

 

Wale ambao si katika jamaa zake wafanye bidii kumuombea maghfira kwa Allaah Aliyetukuka.

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Inafaa Kusafirisha Maiti Kutoka Mji Hadi Mji Mwengine?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share