Anamkataza Mke Wake Apelekwe Hospitali Na Dada Ya Mkewe

SWALI:

 

Assalam Alaykum warahamtullahi wabarakatuh Mdogo wangu anazuiliwa na mumewe kwenda hospitali kutibiwa wakati yeye huyo mumewe hana uwezo wa kumpeleka na mimi ndio nimeamua kumsaidia mdogo wangu aende hospitali kwani hali yake inadhoofika kila siku. Jee naweza kuchukua hatua gani juu ya hili na shem hataki hata kunisikiliza.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu mume kukataa mkewe kusaidiwa na dada yake mkubwa ili apelekwe hospitali kutibiwa.

Hili ni swali ambalo tumelipata upande mmoja bila kusikiliza upande wa pili, wa mume ambao pia nao ni muhimu ili kutoa uamuzi na ufumbuzi muafaka kabisa.

 

Hata hivyo, ikiwa hivyo unavyosema ndivyo sawa na kweli dada yako huyo mdogo yuko katika hali mahututi itabidi umuokoe maisha yake kwa kumpeleka hospitali kisha mtatue matatizo yaliyoko baina yenu kwa njia iliyo nzuri.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share