Wali Wa Kisomali Na Nyama Ya Ng’ombe (Sughaar)

Wali Wa Kisomali Na Nyama Ya Ng’ombe (Sughaar)

  

  

Vipimo vya Sughaar (nyama ng’ombe bila mifupa ilokatwakatwa – beef steak cubes)

Steki ya ng’ombe - 2Lb

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 2

Tangawizi mbichi na kitunguu saumu - 2 vijiko vya chai

Jira/cumin (bizari ya pilau) - 1 kijiko cha chai

Dania/coriander/gilgilani - 1 kijiko cha chai

Pilipili boga la kijani/jekundu - 1

Karoti ilokatwakatwa vipande (cubes) - 1

Njegere za kijani (green peas) - ½ kikombe

Njegere changa (spring beans) - ½ kikombe

Viazi vilokatwakatwa vipande (cubes) - 2

Pilipili mbichi zilokatwakatwa (Chopped) - 2

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Maji - 2 vikombe

Chumvi - Kiasi                                                                         

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.   Weka sufiria katika moto, tia mafuta kisha kaanga nyama kidogo pamoja na

2.   tangawizi mbichi, kitunguu thomu, chumvi, jira na dania.

3.   Tia maji, funika acha ichemke hadi ikaribie kuiva.

4.   Supu ikiwa imebakia nyingi, ipungue iache kando kuitumia katika wali.

5.   Tia karoti, njegere zote, viazi, pilipili boga, pilipili mbichi iache katika moto huku ukikoroga. 

6.   Acha ipikike kwa muda mdogo tu, karibu na mwisho tia vitunguu na changanya vizuri viive kwa mvuke wake.

 

Vipimo vya Wali

Mchele 3 – 4 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 1 uwa

Kotimiri - 3 misongo (bunches)

Mafuta - ¼ kikombe kidogo

Kidonge cha supu (cube stock) - 2

Zaafarani au rangi ya biriani ya manjano - Kiasi

Mdalasini - 1 kijiti

Jira/cumin/bizari pilau - 1 kijiko cha supu

Hiliki - 3 chembe

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1.   Osha mchele na roweka kama ipasavyo kutgemea na aina ya mchele.

2.   Weka sufuria, tia mafuta, kisha tia mchele ukaangekaange kidogo.

3.   Ikiwa utatumia rangi ya biriani, tia katika mchele kidogo tu ugeuke rangi  kiasi.

4.   Saga kitunguu thomu na kotmiri katika mashine ya kusagia (blender) kwa kutia maji kiasi cha kikombe kimoja.

5.   Mimina katika mchele, tia vidonge vya supu, chumvi, kisha ongeza maji kiasi kwa kutegemea aina ya mchele.

6.   Saga jira/cumin tia katika mchele pamoja na mdalasini na chembe za hiliki, funika hadi uive wali ukiwa tayari.

7.   Pakua wali katika sahani kisha weka sughaar juu yake kama ilivyo katika picha au pakua wali na sughaar mbali mbali. Kula kwa ndizi!

                                                           

 

Kidokezo:

1.   Tumia mchele wa Basmati ulio mrefu na kunyooka.

2.   Maji katika mchele yanategemea aina ya mchele. Tumia kiasi tu ili wali utokee mmojammoja usiogandana au usiwe mabonde.

3.   Tolea kwa pilipili mbichi ilosagwa na kitunguu saumu(thomu/galic) na ndimu.

 

 

 

 

 

Share