Anaweza Kuswali Na Damu Inayotoka (Nifasi) Baada Ya Kusafishwa Mimba, Ijapokuwa Hakuzaa

 SWALI:

 Assalaamu alaikum warrahmatullahi wabarakatu

Swali linamtatiza dada yetu kwa kupewa majibu tofauti,swali lenyewe ni hili: Dada amekuwa mja mzito kwa miezi 3, na mimba hiyo ikawa haina mafanikio yaani ikafika wakati mtoto matumboni hakui tena na ikabidi hiyo mimba itolewe. Baada ya dada yetu kusafishwa ikawa damu inatoka kama kawaida ya mwanamke akisha zaa. Jee anaweza kuswali na hiyo damu ijapokuwa hakuzaa?

Jazaakumullahu khairan. wassalaamu alaikum warahmatullahi wabarakatu


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kutoa mimba kwa dada yetu na kuwa bado anatokwa na damu.

Damu hiyo inayomtoka mwanamke aliyeharibu mimba na kisha kusafishwa ni damu ya nifasi. Kwa hiyo hawezi kuswali wala kufunga mpaka isimame kutoka.

Tafadhali bonyeza viungo vifautavyo  upate maelezo na manufaa zaidi:

 Ameharibu Mimba Karibu Na Miezi Mitatu. Je, Damu Inakuwa Ya Aina Gani? Nifaas Au Istihaadhwah?

Mwenye Kuharibu Mimba Na Hukmu Ya Damu Ya Nifaas

Anapoharibu Mimba, Afanye Wudhuu Au Ghuslu?

 Na Allaah Anajua zaidi

 

Share