Ametazama Sinema Chafu Akapatwa Hisia Je Swawm Yake Inakubalika?

SWALI:

Asalam Alaykum

my question is that do i have to make my up fasting again

I hope it clear now

Shukran

First i would like to say thank you all in alhidaaya for making search a great website i learn alote from it ...Now i hope you can help me and my qustion is that i did something very bad but then i realised that i was doing something wrong and same time i,am fasting.  i saw some bad video clips and i got some feelings. what can i do to make it good again? Will my sawm be accepted or i have to pay for it alhought i pray for forgiveness when i realised it was wrong  what can i do to make it good again ,and to get god forgiveness ?

Please it will be very kind of you if i can get the answer as soon as possible

 

 


 

 

JIBU: 

Sifa zote njema anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atutakabalie funga zetu za mwezi Mtukufu wa Ramadhaan na Atudumishe katika mambo mema na ya kheri.

Mwanzo tungependa kuwakumbusha ndugu na dada zetu katika Imani na Uislamu kuwa ni haramu kwa Muislamu kutazama filamu ambazo ni za ngono na chafu ambazo kwayo huamsha hisia na ashiki. Ni vyema kuwa ndugu yetu kaona kuwa lile alilolifanya ni makosa katika Dini. Hii ni neema kwani kutubia itakuwa ni rahisi kwake kuliko mtu anayefanya makosa na akajiona kuwa yuko sawa. Kutazama filamu hizo ni makosa katika Ramadhaan na nje ya Ramadhaan.

Sasa ikiwa kutazama filamu hiyo kulimfanya yeye atokwe na manii, jambo hilo litabatilisha Swawm yake na itabidi siku hiyo asiwe ni mwenye kula wala kunywa kama aliyefunga hadi wakati wa kufungua, na kisha baada ya Ramadhaan itabidi alipe siku moja. Kutokwa na manii kwa kuangalia, au kufikiri sana au kukumbatia au kwa kuvaana kunabatilisha Swawm ya Muislam.

Lau ikiwa hakutokwa na manii kwa kuangalia atakuwa amepata madhambi kwa kufanya kitu cha makosa na itabidi aombe maghfira na asirudie tena kosa hilo. Hivyo hivyo, ikiwa ametokwa na manii itabidi pia aombe maghfira pamoja na kuweka azma ya kutorudia tena kosa hilo na ailipe siku hiyo baada ya Ramadhaan.

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amsamehe ndugu yetu kwa kosa lake hilo alilofanya pamoja na kutusamehe sote makosa mbali mbali tunayofanya mchana na usiku.

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share