Khushuu (Unyenyekevu) Katika Swalah

SWALI:

Je, Swalah yako inapungua daraja mfano ukiwa unawaza kuhusu mambo mengine kwenye Swalah, na hata kama unijitahidi usiwaze chochote isipokuwa kuweka akili yako kwenye Swalah?

 

 


JIBU

Utajitahidi vile unayoweza kuweka mawazo yako yote katika Swalah ili upate "khushuu" (unyenyekevu) wa Swalah ambao ni muhimu sana.  Kwa hiyo utaanza kwa kumlaani ibliys   kusema A'udhu Billahi Mina Shaytaanir-Rajiym.  Swala yako  itakubaliwa hata kama baadhi ya wakati mawazo yako yalikuwa kwengine.  Lakini kila ukiweka mawazo yako kwenye Swalah ndio Swalah inakuwa na thawabu zaidi  na inahesabika zaidi kuwa ni Swalah nzuri yenye kumridhisha Allaah سبحانه وتعالىkama alivyotaja kuwa ni miongoni mwa sifa za watu watakorithi Jannah ya Firdaws. 

قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿1﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿2﴾

1. HAKIKA wamefanikiwa Waumini  

2. Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao  

Al-Mu'minuun 

Ikiwa  Kama  unapoteza kabisa mawazo  wakati wa Swalah nzima basi ni bora  kuirudia Swalah, lakini isiwe mazoea kwani itakuwa ni shetani anakuchezea.

 

Share