Mchuzi Wa Nyama (Trinidad/Guyana)

Mchuzi Wa Nyama (Trinidad/Guyana)

 

  

 

Vipimo

 

Nyama ng’ombe - 1 kilo

Vitunguu  viliokatwakatwa (chop) - 5

Kitunguu saumu(thomu) - 1 uwa au chembe 10

Tangawizi mbichi - ¼ kikombe

Viazi/mbatata viliokatwakatwa vikubwa kwa urefu - 4

Bizari ya mchuzi (curry powder) - 2 vijiko vya supu

Mafuta - ½ kikombe

Nazi (tui) - ½ kikombe

Kotmiri/dania/coriander freshi - 2 mshikamano (bunches)

Maji  - Kiasi cha kuivisha nyama

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka sufuria katika moto, tia mafuta, kasha kaanga kitunguu thomu hadi kigeuke rangi ya hudhurungi. 
  2. Tia bizari ya mchuzi, endelea kukaanga kwa dakika moja. Tia maji vijiko viwili vya supu, kaanga kidogo. 
  3. Tia nyama, koroga ichanganyike vizuri na masala, kishaa kaanga kidogo.   
  4. Tia vitunguu changanya vizuri, kaanga kidogo tu, kisha tia viazi na maji kiasi ya kuivisha nyama.    
  5. Tia chumvi, koroga, funika. 
  6. Karibu na kuiva, tia tangawizi mbichi, kotmiri, tui la nazi, ongezea bizari kidogo ya mchuzi,  iache ichemke kidogo tu.  
  7. Pakua katika chombo ikiwa tayari kuliwa na wali mweupe au roti.

 

Upishi wa roti za ki Tirinidad/Guyana unapatikana katika kiungo kifutacho: 

 

Roti- Chapatti Za Trinidad Na Guyana

 

 

 

 

    

 

Share