Ndoa Ya Muda Kwa Sababu Wanapendana Lakini Hawana Uwezo Wa Kuoana Inajuzu Ndoa Hii?

 

 

SWALI:

 

Su’ali: ikiwa mimi nimemtamani binti kwakufanya naye ijmai na hatutaki kufanya zina awo haramu hal inawezekana tuka owana kimda tu alafu tukafanya mapenzi awo ijmai.kuliko mimi ni lale naye nakumkoseya mungu. nini ndugu zangu mnanisha'uri ao nini nifanye.mana mimi huyo mtoto wakiki nampenda naye ananipenda na uwezo hatuna na kila mmoja anamtamani mwenzake laki adhabu za mungu nikali nasi tuna okopa adhabu hizo tunamuomba mungu asitu adhibu na atukutanishe sote aljanah ferdausi amin. Asalamu 'aleikum

 

 

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ahli zake, Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum jamiy'an) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Tunashukuru kaka yetu kwa swali hili nyeti na ambalo limewatatiza wengi na kuwafanya wengi pia miongoni mwetu kuingia katika mtego kama huo. Inafaa ieleweke kuwa ndoa ya muda imekatazwa kabisa na Mtume Muhammad Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya Vita vya Khaybar kama ilivyonukuliwa na Muslim katika Sahihi yake kutoka kwa ‘Ali bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anh). Ni wakati huo huo ndiyo nyama ya punda pia ilikatazwa. Hivyo, ikiwa utamuoa dada huyo kwa muda inahesabiwa kama umezini naye. Na haingii akilini kuwa umuoe binti huyo kwa muda na kisha umpatie mahitaji yake yote kama malazi, chakula, nguo na vinginezo lakini iwe ukimuoa kihalali ndiyo kuwe na matatizo katika hayo.

 

Mara nyingi huwa tunasumbuliwa na shetani katika kufikiria hivyo. Ikiwa kweli munapendana mutaoana kihalali hivyo kuepukana na adhabu pamoja na ghadhabu ya Allaah. na ikiwa nyinyi ni masikini kama munavyosema lakini munataka kujilinda katika kufanya la haramu kwa kutenda la halali Allaah Atawatolea milango ya kheri katika kila upande. Allaah Anasema: “Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah Atawatajirisha kwa fadhila Yake. Na Allaah ni Mwenye wasaa Mwenye kujua” (24: 32).

 

Kwa hiyo kutokuwa na hali ya kumuoa isiwe ni sababu ya kukuzuwia kumuowa kwani hiyo ni ahadi ya Allaah kwamba Atakutajirisha kwa kutimiza Sunnah hii muhimu.

 

Kwa manufaa zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Ndoa Ya Mut'ah

Hukmu Ya Ndoa Ya Mut'ah

Uthibitisho Wa Makatazo Ya Ndoa Ya Mut’ah

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

Share