Historia Ya Krismasi Na Hukumu Ya Kusherehekea Na Kupongezana

 

Historia Ya Krismasi Na Hukumu Ya Kusherehekea Na Kupongezana

 

Alhidaaya.com

 

 

Historia ya Krismasi

 

Wakati wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii) inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira ya baridi.

 

Wakati wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu nzuri.

 

Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Desemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Desemba.

 

Wakristo wa kale

 

Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristo wa kale walikaa majumbani mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya Wakristo iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua shuruti za Kikristo. Lakini, Makanisa ya kale hakika hayakusherehekea mwezi wa Desemba kwa kuzaliwa Kristo hadi alipokuja Telesforusi Telesphorus, ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136 AD, askofu huyo ndiye aliyetangaza kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili kuadhimisha “Kuzaliwa kwa Bwana wetu na Mwokozi”. Hata hivyo, kwa vile hakuna mtu hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo, kawaida ya Uzawa ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati wa Sherehe za Kiyahudi za Trumpetsi (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300, watu walielewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.

 

Katika mwaka 274 M, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Desemba. Mfalme wa Roma aitwaye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni “Natalis Solis Invicti”, ‘Sherehe Ya Kuzaliwa Jua Lisiloshindikana’. Katika mwaka 320 M, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25 Desemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristo.

 

Mnamo mwaka 325 M, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa maanani. Mtakatifu Constantine, ambaye ni Mfalme wa mwanzo wa dhehebu la Ukristo la Kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiohamishika kwa tarehe 25 Desemba. Pia aliitanguliza Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza (Pasaka) kama ni sherehe yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354 M, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Desemba.

 

Hata hivyo, ingawa Constantine aliifanya rasmi tarehe 25 Desemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitambua kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa Wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni. Huko Uingereza England, Oliver Cromwell alizipiga marufuku sherehe za Krismasi baina ya miaka 1649 na 1660 kupitia kwa inayoitwa Sheria za Rangi Samawati Blue Laws, akiamini kwamba iwe ni siku ya kumuabudu mungu tu.

 

Hamu ya kuifurahia sherehe ya Krismasi ilikirimiwa pale Waprotestanto (Wakristo wasiokubali baadhi ya mafundisho ya Kanisa la Kirumi) walipokimbia uchunguzi kwa kutorokea sehemu za makoloni yote duniani. Hata hivyo, Krismasi bado haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800. Na, weka akilini, hakukuwa na picha ya Baba Krismasi (Santa Claus) kwa wakati huo.

 

Krismasi inaanza kuwa maarufu

 

Umaarufu wa Krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820 kutokana na kitabu cha Washington Irving The Keeping of Christmas at Bracebridge Hall ‘Kuiadhimisha Krismasi Kwenye Jukwaa La Bracebridge’. Mnamo mwaka 1834, Malkia wa Uingereza aitwaye Victoria, alimkaribisha mumewe wa Kijerumani Prince Albert ndani ya Ngome ya Windso Windsor Castle, akimuonesha tamaduni za mti wa Krismasi Christmas tree na Nyimbo Za Kumsifu Yesu Kristo carols ambazo ziliadhimishwa Uingereza kwa Mfalme wa Uingereza. Mwaka 1834, wiki moja kabla ya Krismasi, Charles Dickens alichapisha Nyimbo za Kumsifu Yesu za Krismasi Christmas Carols (ambapo aliandika kwamba Scrooge alimuamrisha Cratchit kufanya kazi, na kwamba Baraza Kuu la Marekani US Congress lilikutana Siku ya Krismasi). Ilikuja kuwa ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za Krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la mwanzo ndani ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mnamo mwaka 1860, mfananishi illustrator wa Marekani aitwaye Thomas Nast alichukua kutoka hadithi za Kiingereza kuhusu Mtakatifu Nicholas, muangalizi mtakatifu wa watoto, kumtengeneza Baba Krismasi Father Christmas. Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama ni sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka, nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu.

 

Nakuombea Krismasi Njema Have a merry Christmas

 

Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya Kikristo yananasibishwa ndani ya Krismasi. Yesu alizaliwa mwezi wa Machi, bado siku yake ya kuzaliwa inasherehekewa Desemba ya 25, wakati wa solstice. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za Krismasi (Desemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisherehekewa na wapagani wa ki-Rumi wakale kwa kuadhimisha kurudi kwa jua. Hivyo, hakuna mshangano wowote kwamba Wakristo waliosafi puritans – au Wakristo wasiotaka mabadiliko conservative – watahamaki kwa Krismasi kuwa “sio ya kidini kama ilivyotakikana kuwa,” wakisahau kwamba Krismasi haikusherehekewa hata kidogo hadi siku za hivi karibuni.

 

Yesu Alisemaje Kuhusu Krismasi?

 

Mazoea ya Krismasi

 

Mti ulio bora wa Krismasi unanunuliwa. Ukipambwa kwa madoido yenye kung’ara pamoja na kumetameta, unasimamishwa karibu na dirisha. Maduka yanajazana wanunuzi wakisaka zawadi na vile viduchu vinasubiri kwa hamu kubwa ya Baba Krismasi Santa.

Ni mshughuliko na ni homa ya Krismasi Christmas fever, umewahi kufikiri kabla? Je, Biblia au Yesu aliwahipo kusababisha homa ya Krismasi?

 

Tafakari juu ya mchanganuo ufuatao kuhusu Krismasi, na ukweli utakuja kuwa wazi zaidi na zaidi.

 

Je, Krismasi Ina Ushahidi wa Biblia?

 

Neno ‘Krismasi’ halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kitu kimoja; upambaji wa mti. Biblia wenyewe inashutumu upambaji wa miti (ya Krismasi):

 

“Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaugandanisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika” (Jeremia 10-3,4).

 

Wazungu wa ki-Pagani kabla ya Ukristo, waliamini miujiza kwamba miti ya kijani ina nguvu maalum za ulinzi. Hakika, matumizi ya Miti ya Krismasi imeanza hivi karibuni tu mwa karne ya 17 huko Strasbourg, Ufaransa na kutoka huko ukaenea hadi Ujerumani, Uingereza na baadaye Marekani. “Ibada ya miti ilikuwa ni jambo la kawaida kwa dini miongoni mwa watu wa Tyutoniki Teutonic na Skandinavia Scandinavia wa Ulaya ya kaskazini kabla ya kuingia kwenye Ukristo…Walowezi wa ki-Jerumani walileta mila za Mti wa Krismasi kwenye makoloni ya Kimarekani mnamo karne ya 17. Kufikia karne ya 19, matumizi yake yalienea sehemu tofauti”. (Angalia Encyclopedia ya Compton, Toleo la 1998)

 

Je, Yesu Alizaliwa Desemba ya 25?

 

Si tarehe ya Desemba 25 wala tarehe nyengine yoyote iliyotajwa ndani ya Biblia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu. Ilikuwa ni hivyo hadi kufikia mwaka 530 C.E kwamba mtawa monk aitwaye Dionysus Exigus, aliweka tarehe isiyobadilika ya kuzaliwa kwa Yesu kuwa ni Desemba 25. “Kulingana na taratibu za ki-Roma, alikosea kuipanga tarehe ya kuzaliwa kwa Kristo (yaani, miaka 754 baada ya kupatikana nchi ya Rumi) kama ni Desemba 25, mwaka 753”. (Angalia: Encyclopedia Britannica, toleo la mwaka 1998) Tarehe hii ilichaguliwa ili iendane pamoja na sikukuu ambazo zimeshagandana na imani za kipagani.

 

Mapagani wa Kirumi walisherehekea Desemba 25 kama ni ya kuzaliwa kwa ‘mungu’ wao wa nuru, aitwaye Mithra.

 

“Mnamo karne ya pili A.D, hiyo sherehe ya Mithra ilikuwa ni ya kawaida zaidi ndani ya Ufalme wa Rumi kuliko Ukristo, ambayo ilizaa mifanano iliyo mingi” (The Concise Columbia Encyclopedia, toleo la mwaka 1995).

 

‘Waungu’ wengine wakipagani waliozaliwa Desemba ya 25 ni: Hercules mtoto wa Zeuz (Wagiriki); Bacchus, ‘mungu’ wa mvinyo (Warumi); Adonis, ‘mungu’ wa Kigiriki, na ‘mungu’ Freyr wa Ugiriki-mapagani wa Roma.

 

Je, Vipi Kuhusu Baba Krismasi Santa Claus?

 

Kama viumbe visivyokuwa binaadamu aliens watafika duniani katika wakati wa Krismasi, bila ya shaka wataamini Krismasi kuwa ni sherehe ya kufurahikia kuzaliwa kwa Baba Krismasi Santa. Majina ya ‘Santa Claus’, hayamo popote ndani ya Biblia.

 

Hata hivyo, Mtakatifu Nikolas Saint Nicholas (Baba Krismasi Santa Claus) alikuwa ni mtu halisi, askofu, ambaye alizaliwa miaka 300 baada ya Yesu. Kwa mujibu wa hekaya za kale, alikuwa ni mtu mwenye huruma mno na alitenga nyakati za usiku kwenda kutoa zawadi kwa mafukara. Baada ya kifo chake mnamo Desemba ya 6, watoto wa shule huko Ulaya walianza kusherehekea siku hiyo kwa karamu kila mwaka.

 

Baadaye Malkia Victoria aliibadilisha sherehe hiyo kutoka Desemba ya 6 kuwa ni Desemba ya 24 kuamkia Krismasi.

 

Je, Yesu au Wafuasi Wake Waliwahi Kusherehekea Krismasi?

 

Kama Yesu alimaanisha kwa wafuasi wake kusherehekea Krismasi, angeliifanyia kazi yeye mwenyewe na kujikusanya pamoja na wafuasi wake. Hakuna sehemu iliyotajwa ndani ya Biblia kwamba kuna mfuasi yeyote aliyewahi kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kama Wakristo wanavyofanya leo.

 

“Kanisa halikupatapo kuweka sikukuu kwa ajili ya sherehe za tukio la Krismasi hadi ilipofika karne ya 4” (Angalia: Encyclopedia ya Grolier)

 

Hivyo, tunaona kwamba sio Biblia wala Yesu na wafuasi wake waliosema kitu kuhusu sherehe za Krismasi ambazo sasa zinahusisha viingilio vya sherehe, biashara, na matumizi yaliyochupa mpaka, ni utovu wa akili kwa mfananisho wowote wa imani.

 

Hukumu Ya Krismasi Na Mwaka Mpya

 

Shukrani Ziende kwa Allaah

 

Shaykh al-Islaam bin Taymiyah (Allaah Amrehemu) alisema kwenye fafanuzi yake katika Aayah (tafsiri ya maana):

وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ

Na wale ambao hawashuhudii uongo, (az-zuur) [Al-Furqaan: 72]

 

Ama kuhusu sherehe za mushrikiyn: wanakusanya pamoja mambo yenye kutia wasiwasi, mahitaji ya mwili na uongo, hakuna chochote ndani yake ambacho kina faida ya kidini, na mwisho wa kutosheleza hizo shahawa, ni maumivu. Hivyo, vitendo vyao ni vya uongo, na kuvishuhudia kunamaanisha kuvifanya. Hii Aayah peke yake inawapandisha daraja na kuwapa moyo (wale ambao hawashuhudii uongo), ambayo ina maana ya kuwahimiza watu kuachana na kushiriki kwenye sherehe zao (mushrikuun) na aina nyenginezo za uongo. Tunafahamu kwamba ni vibaya kushiriki kwenye sherehe zao kwa sababu wanaitwa az-zuur (waongo). Inamaanisha kwamba ni haraam kufanya hivi kwa sababu zilizo nyingi, kwa sababu Allaah Ameiita ni az-zuur.

 

Allaah Anamlaumu yule anayezungumza uongo (az-zuur) hata ikiwa hamna yeyote atakaeathirika nao, kama ilivyo ndani ya Aayah ikikataza Dhwihaar (aina ya talaka ambapo mume anamwambia mkewe “Wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu”), ambapo Yeye Anasema (tafsiri ya maana):

الْقَوْلِ وَزُورًا

Wanasema yasiyokubalika na kauli ya kuchukiza na uongo. [Al-Mujaadilah: 2].

 

Na Allaah Anasema (tafsiri ya maana):

 فَاجْتَنِبُوا الرِّجْسَ مِنَ الْأَوْثَانِ وَاجْتَنِبُوا قَوْلَ الزُّورِ

Basi jiepusheni na uchafu wa (kuabudu) masanamu, na jiepusheni na kauli za uongo. [Al-Hajj: 30].

 

Hivyo yule ambaye anafanya az-zuur analaumiwa kwa mtindo huu. Ndani ya Sunnah:

 

Anas bin Maalik (Allaah Amrehemu) amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuja (Madiynah) na walikuta siku mbili ambazo kipindi cha Jaahiliyyah watacheza (na kujipumzisha).” Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Allaah Amekupeni kilicho bora zaidi kuliko mambo hayo: Yawm adh-Dhuhaa (‘Iyd al-adh haa) na Yawm al-Fitr (‘Iyd al-Fitr).” (Imesimuliwa na Abuu Daawuud).

 

Hii inaonesha wazi kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bila ya shaka alizuia Ummah wake kusherehekea sherehe za kikafiri, na alihakikisha kuziondosha kwa njia zozote zinazowezekana.

 

Ukweli wa kwamba dini ya Watu wa Kitabu inakubaliwa, haina maana kwamba sherehe zao zinakubalika au ziendelezwe na Ummah, kama yalivyo matendo yao mengine ya kikafiri yasivyokubalika, na dhambi zao pia hazikubaliki. Hakika, Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifikia hadi kuamrisha Ummah wake kujitofautisha nao kwenye mambo mengi ambayo ni mubaah (yanaruhusiwa) na kwa taratibu nyingi za ibada, kwa sababu tu; kwamba vinapelekea kuwa sawa nao kwenye mambo mengine pia. Hii kuweka tofauti; ni kuonesha kizuizi katika nyanja zote, kwa sababu namna utakavyokuwa tofauti na watu wa Motoni, ndivyo utakavyokuwa mchache wa kutenda matendo ya watu wa Motoni.

 

Ushahidi wa mwanzo ni Hadiyth ya: “Kila watu wana sherehe zao, na hii ndio sherehe yetu” ambayo ina kusudio maalum kwamba; watu wote wana sherehe zao wenyewe, kama Allaah Anavyosema (tafsiri ya maana):

وَلِكُلٍّ وِجْهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَا ۖ

Na kila mmoja ana upande wa kuuelekea. [Al-Baqarah: 148] na

لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا

Kwa kila (ummah) katika nyinyi Tumeujaalia shariy’ah na manhaj. [Al-Maaidah: 48].

 

Hii inamaanisha kwamba kila taifa lina njia zake wenyewe. Hiyo laam ndani ya li-kulli (“kwa kila”, “katika nyinyi”) ina maana kwa watu maalum. Hivyo, kama Mayahudi wana sherehe na Wakristo wana sherehe, ni za kwao wenyewe, na sisi hatuna sehemu yetu ndani ya hizo sherehe, kama vile tusivyotumia Qiblah kimoja au sheria zao.

 

Ushahidi wa pili ni: masharti aliyoweka ‘Umar bin al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) na kukubaliana pamoja na Swahaabah na Fuqaaha wote baada yao ni: kwa wale Watu wa Kitabu ambao wamekubali kuishi chini ya hukumu za Kiislamu (ahl adh-dhimmah) wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ndani ya Daar al-Islaam (ardhi zilizo chini ya hukumu za Kiislamu). Kama Waislamu wamekubaliana kuwazuia ahl adh-dhimmah kusherehekea wazi wazi, ni namna gani itakuwa sahihi kwa Waislamu kushereheka nao wazi wazi? Kama Muislamu atawasherehekea, jee sio zaidi ya kafiri anavyofanya wazi wazi?

 

Sababu iliyokuwepo ya sisi kuwazuia wasisherehekee sherehe zao wazi wazi ni kwa sababu ya machafu yaliyokuwemo humo. Kwa sababu ya dhambi au alama ya dhambi. Katika kesi yoyote, Muislamu anazuiwa kutenda dhambi au kujaribu kutenda dhambi. Hata kama hakuna uadui wowote kwa Muislamu kuwa nao pamoja katika kusherehekea wazi wazi isipokuwa kafiri kupata nguvu ya kuendelea na matendo yake. Inakuwaje Muislamu anatenda hivyo? Uadui uliokuwemo (ndani ya sherehe zao) utaelezwa chini, insha Allaah.

 

Al-Bayhaqiy amesimulia ikiwa na isnaad swahiyh kwenye Baab karaahiyat ad-dukhuul ‘ala ahl adh-dhimmah fi kanaa’isihim wat-tashabbuh bihim yawmi nawruuzihim wa maharjaanihim (Sura kuhusu karaha ya kuingia kwenye makanisa ya ahl adh-Dhimmah (Makafiri walio katika nchi ya Kiislam)  katika kuadhimisha Mwaka wao Mpya na sherehe nyengine): Kutokana na Sufyaan ath-Thawri na kutokana na Thawr bin Yaziyd na kutokana na ‘Atwa’ bin Diynaar ambao wamesema: ‘Umar amesema: “Musijifunze lugha ya wasiokuwa Waarabu, musiingie pamoja na mushrikiyn kwenye makanisa yao katika siku za karamu zao, kwani laana (za Allaah) zinawashukia juu yao.”

 

‘Umar bin al-Khatwaab amesema:

 

“Jiepusheni na maadui wa Allaah kwenye sherehe zao.” Imesimuliwa kutokana na Abuu Usaamah ikiwa na isnaad iliyo sahihi kwamba: ‘Awn alituambia kutokana na Mughiyrah kutokana na ‘Abdullaah bin ‘Amr: “Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.” ‘Umar alikataza kujifunza lugha zao, na hata kuingia kwenye makanisa yao katika siku ya sherehe yao, jee ni vipi kwa kufanya baadhi ya mambo wanayoyafanya kwenye siku hizo, au kufanya vitu ambavyo ni sehemu ya dini yao? Je, sio kufanya baadhi ya vitu wanavyofanya kwenye sherehe zao ni (uovu) zaidi ya kuingia tu kwenye sherehe zao? Kama laana za Muumba zitaanguka juu yao kwenye siku ya sherehe yao kwa sababu ya yale wanayofanya, je, adhabu hiyo haitokuwa sawa kwa yule anayefanya yale wanayotenda wao, au sehemu ya hayo? Je, sio maneno ya: “Jiepusheni na maadui wa Allaah, kwenye sherehe zao” yana maana kwamba tusikutane nao au kushirikiana nao kwenye siku hizi? Je, ni vipi kwa mtu ambaye hakika anasherehekea sherehe zao?

 

‘Abdullaah bin ‘Amr amesema kwa uwazi:

 

“Yeyote anayeishi ndani ya ardhi ya wasiokuwa Waarabu na kusherehekea Mwaka wao Mpya na sherehe zao, na kujifananisha nao hadi anafariki akiwa na hali hiyo, atakusanywa pamoja nao kwenye Siku ya Malipo.”

 

Hii inamaanisha kwamba yule anayejikusanya nao kwenye mambo yote haya ni kafiri, au kwamba kufanya hivi ni miongoni mwa dhambi kubwa (kabaa’ir) kwamba itampelekea mmoja wao Motoni; maana ya iliyopita ni ile iliyo wazi kutokana na mpangilio wa maneno. Alitaja – Na Allaah Ndie Ajuaye Zaidi – yule anayeishi kwenye ardhi yao, kwa sababu wakati wa ‘Abdullaah bin ‘Amr na Swahaabah wengineo, walikuwa wakizuia sherehe zilizo wazi za kikafiri ndani ya ardhi za Waislamu. Na hakuna Muislamu aliyewaiga kwenye sherehe zao; hilo (la kusherehekea) pale ambapo wanapoishi kwenye ardhi za kikafiri. ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) alikataa hata kulitambua jina la sherehe zao ambazo zilikuwa mahsusi kwa ajili yao, je, itakuwaje kwa kushereheka nao kisawasawa? Ahmad ametaja maana ya simulizi zilizopokelewa kutokana na ‘Umar na ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhuma) kwenye mada hii, na wafuasi wake walijadili masuala ya sherehe.

 

Imaam Abul-Hassan al-‘Aamidiy alisema: mwandishi anayejulikana kwa jina la Ibn al-Baghdaadi alisema ndani ya kitabu chake Umdat al-Haadhwir wa Kifaayat al-Musaafir: “Hairuhusiwi kuingia kwenye sherehe za Wakristo na Mayahudi.” Ahmad alitamka hili kwenye simulizi ya Muhannaa, na ushahidi wake wa hilo ni Aayah (tafsiri ya maana):

 

وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ

Na wale ambao hawashuhudii uongo, [Al-Furqaan: 72]

 

Alisema: (Hizi sherehe ni) ash-Sha’aaniyn pamoja na sherehe zao. Alisema: Waislamu wazuiliwe kuingia kwenye masinagogi (makanisa ya Kiyahudi) na makanisa (ya Wakristo).”

 

Kutokana na Iqtidhwa’ as-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab al-Jahiym iliyoandikwa na Shaykh al-Islaam bin Taymiyah, uk. 183.

 

Kuwatakia kheri ya Krismasi Makafiri na hata sikukuu nyengine za dini tofauti ni haraam kwa mujibu wa makubaliano ya wengi, kama Ibn al-Qayyim (Allaah Amrehemu) alisema kwenye Ahkaam Ahl adh-Dhimmah. 

 

Kuwatakia kheri Makafiri katika mwenendo ambao ni kwa ajili yao ni haraam kwa makubaliano ya wengi, kama ilivyo haraam kuwatakia kheri katika sherehe zao na funga zao kwa kusema ‘Kila la kheri katika sherehe’ au ‘Nakutakia sherehe njema’, na mengineyo. Hata kama yule anayesema haya ameepushwa na ukafiri, lakini bado imekatazwa. Ni kama vile kumpa hongera mtu kwa kuuhami msalaba, au zaidi ya hivyo. Ni kama mfano wa dhambi iliyo kubwa sawa na kumpa hongera mnywaji ulevi, au kumuua mtu, au kuwa na mahusiano ya kinyama, na mengineyo. Wengi miongoni mwa wasio na heshima ya dini yao wanaangukia kwenye kosa hili; hawakai kufikiria ubaya wa vitendo vyao. Yeyote anayempa hongera mtu kwa kutovukwa na adabu au bid’ah au ukafiri amejiweka wazi na laana pamoja na ghadhabu za Allaah.”

 

Kuwapatia hongera makafiri kwenye sherehe za kidini ni haraam kama alivyokwenda mbali Ibn al-Qayyim kwa kufananisha na kwamba yule anayetoa salamu hizo amekubali au ameidhinisha matendo yao ya kikafiri, hata kama mtu hatovifanya mwenyewe vitu hivyo. Lakini Muislamu asikubali mienendo ya kikafiri wala kumpa hongera yeyote kwa ajili yao, kwa sababu Allaah hakubali matendo yoyote kati ya hayo, kama Alivyosema (tafsiri ya maana):

 

إِن تَكْفُرُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنكُمْ ۖ وَلَا يَرْضَىٰ لِعِبَادِهِ الْكُفْرَ ۖ

Mkikufuru, basi hakika Allaah ni Mkwasi kwenu, na wala Haridhii kufuru kwa waja Wake. Na mkishukuru Huridhika nanyi. [Az-Zumar 39:7]

 

 الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekuridhieni Uislamu uwe Dini yenu. [Al-Maaidah:3]

 

Hivyo kuwapa hongera kunazuiwa, hata ikiwa ni mwenzio kazini au vyenginevyo. Kama wao watatutakia kheri kwa kuadhimisha sherehe zao, hatutakiwi kujibu, kwasababu hizi sio sherehe zetu, na kwasababu sio sherehe ambazo zinakubalika na Allaah. Sherehe hizi ni uzushi ndani ya dini zao, na hata zile ambazo zimetajwa huko kabla zimetenguliwa na dini ya Kiislamu, ambayo Ameileta Allaah kwa wanaadamu wetu kupitia kwa bwana Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah Anasema (tafsiri ya maana):

 

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Aal-‘Imraan: 85]

 

Ni haraam kwa Muislamu kukubali mialiko katika sherehe kama hizo, kwa sababu ni zaidi ya kuwatakia kheri kama inavyoonesha kushiriki katika sherehe zao. Vile vile, Waislamu wanazuiwa kuwaiga makafiri katika kuadhimisha huko kwa kushiriki kwenye tafrija parties, au kwa kubadilishana zawadi, au kutoa peremende au chakula, au kuacha kufanya kazi, n.k. Kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema “Yeyote anayewaiga watu ni mmoja wao.”

 

Shaykh al-Islaam bin Taymiyah amesema ndani ya kitabu chake Iqtidhwaa’ as-Swiraat al-Mustaqiym Mukhaalifat Aswhaab Al-Jahiym:

 

“Kuwaiga katika baadhi ya sherehe zao inamaanisha kwamba mtu amefurahia imani zao za uongo na vitendo vyao, na anawapa matumaini kwamba wanaweza kuwa na nafasi ya kuwanyanyasa na kuwapeleka ovyo wanyonge.” Yeyote anayefanya mambo kama haya ni mtenda dhambi, ikiwa anafanya kwa ukarimu au urafiki, au kwa sababu anaona hayaa kukataa, au kwa sababu nyengine yoyote. Kwa sababu ni unafiki ndani ya Uislamu, na kwa sababu inawafanya makafiri kujisikia fakhari kwa dini yao.

 

Allaah Pekee ndiye tunayemuomba kuwafanya Waislamu kuwa fakhari na dini yao, kuwasaidia kuwa thaabiti katika kushikamana na dini yao, na kuwafanya kuwa washindi dhidi ya maadui zao, kwani Yeye Mwenye Nguvu ndiye Mwenye Kuweza.

 

Share