Mashairi: Allaah Awanusuru Syria Na Myanmar (Burma)

         ‘Abdallaah Bin Eifan
        (Jeddah, Saudi Arabia)

                          (A)

 

Kwa jina Lake Mwenyezi, Mola wetu Subhana,

Nawasalimu Wapenzi, Awalinde Maulana,

Yeye ndie Mkombozi, Peke Yake hana mwana,

Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

 

Manusayri makafiri, Syria wanapigana,

Mashia hawa hatari, hawajui uungwana,

Wao wanapenda shari, wanapenda kuuana,

Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

 

Ni maadui wa Sunni, yote yanaonekana,

Huwachinja Waumini, kwa silaha kila aina,

Silaha toka Irani, na Urusi na Uchina,

Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

 

Waumini siku hizi, Syria wana shida sana,

Wamekuwa Wakimbizi, hata chakula hawana,

Wengine hawajiwezi, wanakufa tunaona,

Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

 

Manusayri mashetani, makafiri wajalana,

Hawafungi Ramadhani, wala Kuhiji hapana,

Dini yao sio dini, na Pagani hufanana,

Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

 

Allah Awape subira, watoto wanalizana,

Wanarusha makombora, kwa marefu na mapana,

Mabinti hutekwa nyara, nashindwa hata kunena,

Mungu Awaangamize, Manusayri makafiri.

 

 

                           (B)

 

Kwingine ni Myanmari, wanapigwa Waumini,

Tunakuomba Qahari, Rudisha kwao amani,

Watoe kwenye hatari, wamo kwenye mtihani,

Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

 

Mabudha wa Myanmari, Burma jina la zamani,

Watose kwenye bahari, kama vile Fira’auni,

Uvunje yao kiburi, na vichwa virudi chini,

Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

 

Na tena bila futari, walifunga Ramadhani,

Na Wewe ndio Jabari, Unawaona Machoni,

Faraji wanasubiri, kutoka Kwako mbinguni,

Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

 

Umoja wa Mataifa, wananyamaza kwa nini?

Sababu wanaokufa, ni Waislamu yakini,

Twazijua zao sifa, na chuki kwa yetu dini,

Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

 

Tuamke Waislamu, na macho yafumbueni,

Imani iwe timamu, masikio zibueni,

Walimu na Maimamu, watoto wazindueni,

Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

 

Kweli nina wasiwasi, ndugu wapo hatarini,

Ninamuomba Mkwasi, Awalinde masikini,

Ombeni duaa upesi, kwenye Swalah ziombeni,

Mungu Awaangamize, Mabudha wa Myanmari.

 

Share