019 - Maryam

  مَرْيَم

 

019-Maryam

 

 

019-Maryam: Utangulizi Wa Suwrah

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

كهيعص ﴿١﴾

1. Kaaf Haa Yaa ‘Ayn Swaad.[1]

 

 

 

ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا ﴿٢﴾

2. (Huu ni) ukumbusho wa Rehma ya Rabb wako kwa Mja Wake Zakariyyaa.  

 

 

 

إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا ﴿٣﴾

3. Alipomwita Rabb wake mwito wa siri.

 

 

 

قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا ﴿٤﴾

4. Akasema: Rabb wangu! Hakika mimi mifupa imeninyong’onyea na kichwa kimeng’aa mvi, na wala sikuwa mwenye kunyimwa katika kukuomba Duaa, ee Rabb wangu.[2]

 

 

 

وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِن وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا ﴿٥﴾

5. Nami nakhofia jamaa zangu nyuma yangu, na mke wangu ni tasa. Basi Nitunukie kutoka kwako (mwana) mrithi.[3]

 

 

 

يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا ﴿٦﴾

6. Anirithi na arithi kizazi cha Ya’quwb, na Mjaalie Rabb wangu awe mwenye kuridhisha

 

 

 

يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ﴿٧﴾

7. (Akaambiwa): Ee Zakariyyaa! Hakika Sisi Tunakubashiria ghulamu jina lake Yahyaa, Hatukupata kabla kumpa jina hilo yeyote.  

 

 

 

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا ﴿٨﴾

8. (Zakariyyaa) akasema: Ee Rabb wangu! Vipi nitapata ghulamu na hali mke wangu ni tasa, na nimeshafikia uzee wa kupindukia mipaka?  

 

 

 

قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْئًا ﴿٩﴾

9. Akasema: Ni hivyo hivyo (lakini) Rabb wako Amesema: Haya ni sahali Kwangu kwani Nilikwishakukuumba kabla na wala hukuwa chochote.

 

 

 

قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۚ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ لَيَالٍ سَوِيًّا ﴿١٠﴾

10. (Zakariyyaa) akasema: Rabb wangu! Nijaalie Aayah (Ishara, Alama). Akasema: Aayah yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu nyusiku tatu ilhali huna kasoro.

 

 

 

فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿١١﴾

11. Basi akawatokea watu wake kutoka mihrabuni, akawaashiria: Msabihini (Allaah) asubuhi na jioni.

 

 

 

يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا ﴿١٢﴾

12. Ee Yahyaa!  Chukua Kitabu kwa nguvu. Na Tukampa Hikmah angali mtoto.

 

 

 

وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً ۖ وَكَانَ تَقِيًّا ﴿١٣﴾

13. Na (Tukampa pia) upole na huruma kutoka Kwetu, na utakaso (pia), na akawa mwenye taqwa. 

 

 

 

وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا ﴿١٤﴾

14. Na mtiifu mno kwa wazazi wake wawili, na wala hakuwa jabari wala muasi.

 

 

 

وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا ﴿١٥﴾

15. Na amani iwe juu yake siku aliyozaliwa, na siku atakayokufa na siku atakayofufuliwa kuwa hai.

 

 

 

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا ﴿١٦﴾

16. Na mtaje katika Kitabu Maryam[4] alipojiondosha kutoka kwa ahli zake, mahali pa Mashariki.

 

 

 

فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ﴿١٧﴾

17. Akafanya pazia kujitenga nao, Tukampelekea Ruwh[5] Wetu (Jibriyl عليه السلام) akajimithilisha kwake kama binaadam timamu.

 

 

 

قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَـٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا ﴿١٨﴾

18. (Maryam) akasema: Najikinga kwa Ar-Rahmaan usinidhuru, ukiwa ni mwenye taqwa.

 

 

 

قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا ﴿١٩﴾

19. (Jibriyl عليه السلام) akasema: Hakika mimi ni Mjumbe wa Rabb wako ili nikubashirie tunu ya ghulamu aliyetakasika.

 

 

 

قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا ﴿٢٠﴾

20. (Maryam) akasema: Itakuwaje niwe na ghulamu na hali hakunigusa mtu yeyote, na wala mimi si kahaba?

 

 

 

قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا ﴿٢١﴾

21. (Jibriyl) akasema: Ni hivyo hivyo (lakini) Rabb wako Amesema: Haya ni sahali Kwangu! Na ili Tumfanye awe Aayah (Ishara, Alama, Dalili) kwa watu na Rahmah kutoka Kwetu, na limekuwa jambo lililokwisha hukumiwa.

 

 

 

فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا ﴿٢٢﴾

22. Basi akaibeba mimba, na akaondoka nayo mahali pa mbali.

 

 

 

فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَـٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا ﴿٢٣﴾

23. Uchungu wa uzazi ukampeleka mpaka katika shina la mtende. Akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya na nikawa niliyesahaulika kabisa!

 

 

 

فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا ﴿٢٤﴾

24. (Jibriyl au ‘Iysaa) akamnadia kutoka chini yake kwamba: Usihuzunike! Rabb wako Amekwishakufanyia kijito cha maji.

 

 

 

وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾

25. Na tingisha kuelekea kwako shina la mtende, litakuangushia tende safi zilizoiva na zilizo tayari kuchumwa.

 

 

 

فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَـٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا ﴿٢٦﴾

26. Basi kula na kunywa na litue jicho lako. Na utakapokutana na mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri ya kunyamaza kwa Ar-Rahmaan, hivyo leo sitomsemesha mtu yeyote.

 

 

 

فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا فَرِيًّا ﴿٢٧﴾

27. Akawafikia watu wake akiwa amembeba (mtoto), wakasema: Ee Maryam! Kwa yakini umeleta jambo la ajabu, kuu na ovu mno! 

 

 

 

يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا ﴿٢٨﴾

28. Ee dada wa Haaruwn! Hakuwa baba yako mtu muovu, na wala hakuwa mama yako kahaba.

 

 

 

فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا ﴿٢٩﴾

29. Akamuashiria. Wakasema: Vipi tuseme na aliye kwenye susu (kitanda) akiwa bado ni mtoto mchanga?

 

 

 

قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّـهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا ﴿٣٠﴾

30. (Mtoto huyo ‘Iysaa) akasema:[6] Hakika mimi ni Mja wa Allaah, Amenipa Kitabu (Injiyl) na Amenijaalia kuwa Nabiy.[7]

 

 

 

وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ مَا دُمْتُ حَيًّا ﴿٣١﴾

31. Na Amenijaalia kuwa mwenye kubarikiwa popote nitakapokuweko, na Ameniusia Swalaah na Zakaah madamu niko katika uhai.

 

 

 

وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا ﴿٣٢﴾

32. Na niwe mtiifu kwa mama yangu, na wala Hakunijaalia kuwa jabari, mwovu.

 

 

 

وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا ﴿٣٣﴾

33. Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.

 

 

 

ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ ﴿٣٤﴾

34. Huyo ndiye ‘Iysaa mwana wa Maryam! Kauli ya haki ambayo wanaitilia shaka.

 

 

 

 

مَا كَانَ لِلَّـهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ ۖ سُبْحَانَهُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٣٥﴾

35. Haiwi kwa Allaah kamwe Ajichukulie mwana yeyote. Subhaanah! (Utakasifu ni Wake!) Anapokidhia jambo basi huliambia: Kun! (Kuwa) nalo linakuwa!

 

 

 

وَإِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٣٦﴾

 

36. (Nabiy ‘Iysaa akasema): Na kwamba hakika Allaah Ni Rabb wangu, na Rabb wenu, basi mwabuduni Yeye (Pekee). Hii ndio njia iliyonyooka.

 

 

 

فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٣٧﴾

37. Lakini makundi yakakhitilafiana baina yao (kuhusu Nabiy ‘Iysaa).  Basi ole wao wale waliokufuru na hudhurisho la Siku iliyo kuu kabisa.[8]

 

 

 

أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَـٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿٣٨﴾

38. Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayotujia. Lakini madhalimu hivi sasa wako katika upotofu ulio bayana.

 

 

 

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ ﴿٣٩﴾

39. Na waonye Siku ya majuto itakapohukumiwa amri, na hali wao wamo katika mghafala, wala hawaamini.

 

 

 

إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ ﴿٤٠﴾

40. Hakika Sisi Tutairithi ardhi na waliokuwemo humo, na Kwetu watarejeshwa.

 

 

 

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٤١﴾

41. Na mtaje katika Kitabu Ibraahiym. Hakika yeye alikuwa mkweli wa kidhati, Nabiy.

 

 

 

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا ﴿٤٢﴾

42. Pindi alipomwambia baba yake: Ee baba yangu kipenzi! Kwa nini unaabudu vile visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa kitu chochote?

 

 

 

يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا ﴿٤٣﴾

43. Ee baba yangu kipenzi! Hakika mimi imekwishanijia elimu isiyokufikia wewe, basi nifuate nikuongoze njia iliyonyooka.

 

 

 

يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَـٰنِ عَصِيًّا ﴿٤٤﴾

44. Ee baba yangu kipenzi! Usimwabudu shaytwaan. Hakika shaytwaan daima ni mwenye kumuasi Ar-Rahmaan.

 

 

 

يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا ﴿٤٥﴾

45. Ee baba yangu kipenzi! Hakika mimi nakhofu isije kukushika adhabu kutoka kwa Ar-Rahmaan, ukaja kuwa rafiki wa shaytwaan.  

 

 

 

قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا ﴿٤٦﴾

46. (Baba yake) akasema: Unachukia waabudiwa wangu ee Ibraahiym? Usipokoma, basi lazima nitakupiga mawe, na niondokelee mbali kwa muda mrefu!

 

 

 

قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا ﴿٤٧﴾

47. (Ibraahiym) akasema: Salaamun ‘Alayka. (Amani iwe juu yako). Nitakuombea maghfirah kwa Rabb wangu. Hakika Yeye daima Ni Mwenye Kunihurumia sana.

 

 

 

وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا ﴿٤٨﴾

48. Na natengana nanyi na mnavyoviomba badala ya Allaah. Na namuomba Rabb wangu, asaa nisijekuwa mwenye kunyimwa duaa yangu kwa kumwomba Rabb wangu.

 

 

 

فَلَمَّا اعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ وَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا ﴿٤٩﴾

49. Basi alipotengana nao na wanayoyaabudu badala ya Allaah, Tulimtunukia Is-haaq, na (mjukuu) Ya’quwb. Na kila mmoja wao Tulimjaalia kuwa Nabiy.

 

 

 

وَوَهَبْنَا لَهُم مِّن رَّحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا ﴿٥٠﴾

50. Na Tukawatunukia katika Rehma Zetu, na Tukawajaalia wenye kutajwa kwa sifa nzuri za kutukuka.

 

 

 

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَىٰ ۚ إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥١﴾

51. Na mtaje katika Kitabu Muwsaa. Hakika yeye alikuwa amekhitariwa kwa ikhlaasw yake na alikuwa Rasuli na Nabiy.

 

 

 

وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا ﴿٥٢﴾

52. Na Tukamwita kutoka upande wa kulia wa mlima na Tukamkurubisha kuzungumza naye kwa siri.

 

 

 

وَوَهَبْنَا لَهُ مِن رَّحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيًّا ﴿٥٣﴾

53. Na Tukamtunukia kutokana na Rehma Zetu, kaka yake Haaruwn awe Nabiy.

 

 

 

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ﴿٥٤﴾

54. Na mtaje katika Kitabu Ismaa’iyl. Hakika yeye alikuwa mkweli wa ahadi na alikuwa Rasuli na Nabiy.

 

 

 

وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ مَرْضِيًّا ﴿٥٥﴾

55. Na alikuwa akiwaamrisha ahli zake Swalaah na Zakaah, na alikuwa mridhiwa mbele ya Rabb wake.

 

 

 

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا ﴿٥٦﴾

56. Na mtaje katika Kitabu Idriys. Hakika yeye alikuwa mkweli wa kidhati, Nabiy.

 

 

 

وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا﴿٥٧﴾

57. Na Tukamuinua daraja ya juu.

 

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُ الرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩﴿٥٨﴾

58. Hao ndio ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii katika uzao wa Aadam, na wale Tuliowapandisha (katika jahazi) pamoja na Nuwh[9] na katika uzao wa Ibraahiym na (uzao wa) Israaiyl (Ya’quwb) na wale Tuliowaongoa na Tukawateua. Wanaposomewa Aayaat za Ar-Rahmaan huporomoka kifudifudi wakisujudu na kulia.

 

 

 

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا ﴿٥٩﴾

59. Wakafuata baada yao waovu, walipoteza Swalaah na wakafuata matamanio, basi watakutana na adhabu motoni.

 

 

 

إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا ﴿٦٠﴾

60. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akatenda mema. Basi hao wataingia Jannah na wala hawatodhulumiwa chochote.

 

 

 

جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدَ الرَّحْمَـٰنُ عِبَادَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّهُ كَانَ وَعْدُهُ مَأْتِيًّا ﴿٦١﴾

61. Jannaat za kudumu milele ambazo Ar-Rahmaan Amewaahidi Waja Wake bila wao kuziona. Hakika Ahadi Yake itafika tu.

 

 

 

لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَامًا ۖ وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ﴿٦٢﴾

62. Hawatosikia humo upuuzi wowote ule isipokuwa salama tu. Na watapata riziki zao humo asubuhi na jioni.

 

 

 

تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيًّا ﴿٦٣﴾

63. Hiyo ni Jannah ambayo Tutawarithisha miongoni mwa Waja Wetu waliokuwa na taqwa.

 

 

 

وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا ﴿٦٤﴾

64. Na (sisi Malaika) hatuteremki ila kwa Amri ya Rabb wako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Ni Yake Yeye yaliyoko mbele yetu, na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyoko baina ya hayo. Na Rabb wako Si Mwenye Kusahau kamwe.[10]

 

 

 

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

65. Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?[11]

 

 

وَيَقُولُ الْإِنسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا ﴿٦٦﴾

66. Na binaadam husema: Je, nitakapokufa, hivi kweli nitatolewa nikiwa hai?

 

 

 

أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا ﴿٦٧﴾

67. Je, hakumbuki binaadam kwamba Tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?

 

 

 

فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا ﴿٦٨﴾

68. Basi Naapa kwa Rabb wako. Bila shaka Tutawakusanya wao pamoja na mashaytwaan, kisha Tutawahudhurisha pembezoni mwa Jahannam huku wamepiga magoti.

 

 

 

ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَـٰنِ عِتِيًّا ﴿٦٩﴾

69. Kisha bila shaka Tutawachomoa kutoka katika kila kundi wale ambao walimuasi zaidi Ar-Rahmaan.

 

 

 

ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا ﴿٧٠﴾

70. Kisha bila shaka Sisi Tunawajua zaidi wale wanaostahiki zaidi kuunguzwa humo.

 

 

 

وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا ﴿٧١﴾

71. Na hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ni mwenye kuufikia (moto).[12] Hiyo ni hukumu ya Rabb wako lazima itimizwe.  

 

 

 

ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا ﴿٧٢﴾

72. Kisha Tutawaokoa wale waliokuwa na taqwa, na Tutawaacha madhalimu humo wamepiga magoti.

 

 

 

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا أَيُّ الْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَّقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا ﴿٧٣﴾

73. Na wanaposomewa Aayaat Zetu zilizo wazi, wale waliokufuru huwaambia walioamini: Kundi lipi kati ya mawili haya lenye cheo bora zaidi na majilisi mazuri zaidi?

 

 

 

وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَاثًا وَرِئْيًا ﴿٧٤﴾

74. Ni karne nyingi sana Tumeziangamiza kabla yao. Wao walikuwa na mapambo mazuri zaidi na mwonekano maridadi zaidi.

 

 

 

قُلْ مَن كَانَ فِي الضَّلَالَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ الرَّحْمَـٰنُ مَدًّا ۚ حَتَّىٰ إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ إِمَّا الْعَذَابَ وَإِمَّا السَّاعَةَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضْعَفُ جُندًا ﴿٧٥﴾

75. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Aliyekuwa katika upotofu, basi Ar-Rahmaan Atawapanulia muda. Hata watakapoona waliyotishiwa; ima adhabu au ima Saa, basi watakuja kujua ni nani aliye mahali paovu zaidi na mwenye askari dhaifu.

 

 

 

وَيَزِيدُ اللَّـهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَّرَدًّا ﴿٧٦﴾

76. Na Allaah Atawazidishia hidaaya wale wenye kushika uongofu. Na mema yanayobakia[13] ni bora zaidi mbele ya Rabb wako kwa thawabu na matokeo bora zaidi ya mwisho.

 

 

 

أَفَرَأَيْتَ الَّذِي كَفَرَ بِآيَاتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا ﴿٧٧﴾

77. Je, umemuona yule aliyezikufuru Aayaat Zetu na akasema: Bila shaka nitapewa (Aakhirah) mali na watoto?[14]

 

 

 

أَطَّلَعَ الْغَيْبَ أَمِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ﴿٧٨﴾

78. Je, kwani ameyajua ya ghaibu au amechukua ahadi kwa Ar-Rahmaan?

 

 

 

كَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُ مِنَ الْعَذَابِ مَدًّا ﴿٧٩﴾

79. Laa, hasha! Tutayaandika yale anayoyasema na Tutampanulia muda wa adhabu ya kurefuka.

 

 

 

وَنَرِثُهُ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا ﴿٨٠﴾

80. Na Tutamrithi yale anayoyasema (mali na watoto), na atatujia peke yake!

 

 

 

وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ آلِهَةً لِّيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا ﴿٨١﴾

81. Na wakachukua badala ya Allaah waabudiwa ili eti iwape taadhima na nguvu.

 

 

 

كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا ﴿٨٢﴾

82. Laa, hasha! Watakanusha ibaada zao, na watakuwa wapinzani wao.

 

 

 

أَلَمْ تَرَ أَنَّا أَرْسَلْنَا الشَّيَاطِينَ عَلَى الْكَافِرِينَ تَؤُزُّهُمْ أَزًّا ﴿٨٣﴾

83. Je, huoni kwamba Sisi Tunapeleka mashaytwaan kwa makafiri ili wawachochee (uovu) kwa uchochezi?

 

 

 

فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا ﴿٨٤﴾

84. Basi usiwafanyie haraka. Hakika Sisi Tunawahesabia idadi za (siku) zao.

 

 

 

يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَـٰنِ وَفْدًا ﴿٨٥﴾

85. Siku Tutakayowakusanya wenye taqwa kwenda kwa Ar-Rahmaan wakiwa (juu ya vipando) kama ni wawakilishi wa heshima.

 

 

 

وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا ﴿٨٦﴾

86. Na Tutawaendesha wahalifu kuelekea Jahannam wakiwa na kiu.

 

 

 

لَّا يَمْلِكُونَ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ﴿٨٧﴾

87. Hawatokuwa na mamlaka ya shufaa isipokuwa yule aliyechukua ahadi kwa Ar-Rahmaan.

 

 

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ﴿٨٨﴾

88. Na wamesema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana.[15]

 

 

 

لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا ﴿٨٩﴾

89. Kwa yakini mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno!

 

 

 

تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾

90. Zinakaribia mbingu kupasuka kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka![16]

 

 

 

أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا ﴿٩١﴾

91. Kwa kule kudai kwao kuwa Ar-Rahmaan Ana mwana.

 

 

 

وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَـٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا ﴿٩٢﴾

92. Na wala haipasi kwa Ar-Rahmaan Kujifanyia mwana.

 

 

 

إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا ﴿٩٣﴾

93. Hakuna yeyote yule aliyeko katika mbingu na ardhi isipokuwa atamjia Ar-Rahmaan akiwa ni mtumwa Kwake.

 

 

 

لَّقَدْ أَحْصَاهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا ﴿٩٤﴾

94. Kwa hakika Amewadhibiti barabara, na Akawahesabu hesabu ya sawasawa.

 

 

 

وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْدًا ﴿٩٥﴾

95. Na kila mmoja wao atamjia (Allaah) Siku ya Qiyaamah akiwa peke yake.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَـٰنُ وُدًّا ﴿٩٦﴾

96. Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Ar-Rahmaan Atawajaalia kwao mapenzi.

 

 

 

فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ الْمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِ قَوْمًا لُّدًّا ﴿٩٧﴾

97. Basi hakika Tumeiwepesisha (Qur-aan) kwa lugha yako ili uwabashirie kwayo wenye taqwa, na uwaonye kwayo watu makhasimu.

 

 

 

 

وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هَلْ تُحِسُّ مِنْهُم مِّنْ أَحَدٍ أَوْ تَسْمَعُ لَهُمْ رِكْزًا ﴿٩٨﴾

98. Na ni karne nyingi sana Tumeziangamiza kabla yao. Je unamhisi hata mmoja katika wao, au unasikia mchakato wowote wao?

 

 

 

 

 

[1] الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).

 

[2] Kutawassal Katika Duaa Kwa Hali Na Sababu Ya Kutaka Duaa Itaqabaliwe:

 

Aayah hii ya (3) hadi namba (6), Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام)  anatawassal (anajikurubisha kwa Allaah) wakati anapoomba duaa yake hii kwa kutaja hali yake ilivyo ya siha na uzee pamoja na mkewe kwamba ni tasa.  Na akataja sababu ya kuhitaji haja yake, nayo ni kuomba mtoto ili amrithi.  Akataja kwanza mifupa yake kuwa dhaifu na nywele zake kugeuka mvi. Kisha akataja sababu kwamba alikhofu baada ya kufariki kwake kubakia kizazi kiovu, hivyo aliomba mtoto ili awe Nabiy baada yake atakayeongoza watu katika Dini. Hivyo basi, kutaja sababu na kujieleza kwa Allaah wakati wa kuomba duaa ya mas-ala ya kidunia na kiaakhirah, ni jambo linaloruhusiwa madam tu ni jambo lenye kumridhisha Allaah (سبحانه وتعالى).   

 

[3] Urithi Wa Unabii Ni Wa Ilimu Na Kulingania Dini: 

 

Kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth:

 

وَإنَّ العُلَمَاءَ وَرَثَةُ الأنْبِيَاءِ ، وَإنَّ الأنْبِيَاءَ لَمْ يَوَرِّثُوا دِينَاراً وَلاَ دِرْهَماً وَإنَّمَا وَرَّثُوا العِلْمَ ، فَمَنْ أَخَذَهُ أَخَذَ بحَظٍّ وَافِرٍ. رواه أَبُو داود والترمذي .

Na hakika ‘Ulamaa ni warithi wa Manabii. Na hakika Manabii hawarithi dinari wala dirham, na bila shaka wao hurithiwa ilimu. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

[4] Fadhila Za Maryam Mama Wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام):

 

Maryam ni miongoni mwa wanawake bora kabisa wa ulimwengu. Rejea pia Aal-‘Imraan (3:42). Ambamo Allaah (سبحانه وتعالى) Amemtakasa na kumsifia.  Juu ya hayo, Allaah (سبحانه وتعالى) Amemfadhilisha kwa kujaalia Suwrah hii kuwa ni Suwrah pekee ya jina la mwanamke naye ndiye Maryam.

 

 

[5] Maana Za Ruwh Katika Qur-aan:

 

Rejea An-Nahl (16:2).

 

[6] Watoto Wachanga Watatu Walioongea:

 

Kuanzia Aayah hii namba (30) hadi namba (33) kisha namba (35-36) ni kauli ya Nabiy Iysaa (عليه السّلام)  alipokuwa angali mchanga.

 

Na Hadiyth ifuatayo imethibitisha kuongea kwake angali mchanga pamoja na watoto wawili wengineo:

 

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لَمْ يَتَكَلَّمْ فِي الْمَهْدِ إِلاَّ ثَلاَثَةٌ عِيسَى، وَكَانَ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ جُرَيْجٌ، كَانَ يُصَلِّي، فَجَاءَتْهُ أُمُّهُ فَدَعَتْهُ، فَقَالَ أُجِيبُهَا أَوْ أُصَلِّي‏.‏ فَقَالَتِ اللَّهُمَّ لاَ تُمِتْهُ حَتَّى تُرِيَهُ وُجُوهَ الْمُومِسَاتِ‏.‏ وَكَانَ جُرَيْجٌ فِي صَوْمَعَتِهِ، فَتَعَرَّضَتْ لَهُ امْرَأَةٌ وَكَلَّمَتْهُ فَأَبَى، فَأَتَتْ رَاعِيًا، فَأَمْكَنَتْهُ مِنْ نَفْسِهَا فَوَلَدَتْ غُلاَمًا، فَقَالَتْ مِنْ جُرَيْجٍ‏.‏ فَأَتَوْهُ فَكَسَرُوا صَوْمَعَتَهُ، وَأَنْزَلُوهُ وَسَبُّوهُ، فَتَوَضَّأَ وَصَلَّى ثُمَّ أَتَى الْغُلاَمَ فَقَالَ مَنْ أَبُوكَ يَا غُلاَمُ قَالَ الرَّاعِي‏.‏ قَالُوا نَبْنِي صَوْمَعَتَكَ مِنْ ذَهَبٍ‏.‏ قَالَ لاَ إِلاَّ مِنْ طِينٍ‏.‏ وَكَانَتِ امْرَأَةٌ تُرْضِعُ ابْنًا لَهَا مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَمَرَّ بِهَا رَجُلٌ رَاكِبٌ ذُو شَارَةٍ، فَقَالَتِ اللَّهُمَّ اجْعَلِ ابْنِي مِثْلَهُ‏.‏ فَتَرَكَ ثَدْيَهَا، وَأَقْبَلَ عَلَى الرَّاكِبِ فَقَالَ اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلْنِي مِثْلَهُ‏.‏ ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَى ثَدْيِهَا يَمَصُّهُ ـ قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم يَمَصُّ إِصْبَعَهُ ـ ثُمَّ مُرَّ بِأَمَةٍ فَقَالَتِ اللَّهُمَّ لاَ تَجْعَلِ ابْنِي مِثْلَ هَذِهِ‏.‏ فَتَرَكَ ثَدْيَهَا فَقَالَ اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِثْلَهَا‏.‏ فَقَالَتْ لِمَ ذَاكَ فَقَالَ الرَّاكِبُ جَبَّارٌ مِنَ الْجَبَابِرَةِ، وَهَذِهِ الأَمَةُ يَقُولُونَ سَرَقْتِ زَنَيْتِ‏.‏ وَلَمْ تَفْعَلْ ‏"‏‏.‏

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hawakuzungumza mbelekoni ila watu watatu: (Mtoto wa kwanza ni) ‘Iysaa. (Mtoto wa pili ni mtoto) katika wana wa Israaiyl kulikuwa na mtu akiitwa Jurayj, mtu huyu alikuwa anaswali. Siku moja mama yake akaja akamwita lakini yule Jurayj akawa anawaza kwa kujiuliza: Je, nimjibu mama yangu au niendelee kuswali? Akaamua kuendelea kuswali na hakumjibu mama yake. Mama yake akasema: “Ee Allaah! Usimfishe mpaka umuoneshe nyuso za malaya.” Siku moja Jurayj alikuwa katika nyumba yake ya ibaada akamjia mwanamke, akamueleza anachokitaka (kufanya ya machafu). Jurayj akakataa. Yule mwanamke akaenda kwa mchungaji, na kutoa mwili wake kwake, basi (akashika mimba) na akazaa mtoto mwanamme, baada ya kufanya tendo la ndoa na yule mchungaji. Yule mwanamke akawa anadai kuwa yule mtoto amezaa na Jurayj. Watu wakamjia Jurayj na wakaivunja nyumba yake ya ibaada, na wakamtoa nje na kumtukana. Jurayj akatawadha na akaswali kisha akaenda kwa yule mtoto. Akamuuliza yule mtoto: “Je, baba yako ni nani, ee kijana?” Yule mtoto Akajibu: “Baba yangu ni mchungaji.” Watu baada ya kusikia haya wakamwambia Jurayj: “Tutakujengea nyumba yako kwa dhahabu.”  Jurayj Akajibu: “Hapana, bali nijengeeni kwa udongo.”  (Ama mtoto wa tatu ni)  mwanamke fulani katika Bani Israaiyl ana mnyonyesha mtoto wake, mara akampitia mtu amepanda mnyama, mtu anayeashiriwa kwa hadhi na umaridadi. Yule mama akasema: “Ee Allaah! Mfanye mwanangu awe kama yule.” Yule mtoto akaliacha titi la mama yake akamuelekea yule aliyepanda akasema: “Ee Allaah! Usinijaalie kuwa kama yule!” Kisha akalielekea titi la mama yake huku anaendelea kunyonya.” Abuu Hurayrah ضي الله عنه) akaendelea: Kama vile ninamuangalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anakinyonya kidole chake (akiashiria mtoto alivyokuwa). Kisha baada ya muda watu wakapita wakiwa na mjakazi. Mama yake yule mtoto akasema: “Ee Allaah!  Usimfanye mwanangu kama huyu.” (yaani kama yule mjakazi). Yule mtoto akaliacha titi la mama yakekisha akasema: “Ee Allaah! Nijaalie kuwa kama yule.” Mama akasema: “Kwa nini unasema hivyo?” Yule mtoto akasema: “‘Yule mtu aliyekuwa amepanda ni dhalimu. Ama huyu mjakazi, wale watu wanasema kuwa ameiba, amezini ilhali hakufanya hivyo.” [Al-Bukhaariy Kitaab Cha Hadiyth Za Manabii]

 

[7] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  Anakiri Kuwa Yeye Ni Mja Wa Allaah Na Wala Sio Mwana Au Mshirika Wa Allaah:

 

Aayah hii ya Maryam (30 hadi 36), ni dalili ya wazi kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  ni mja wa Allaah na si mtoto Wake wala mshirika Wake. Rejea pia Az-Zukhruf (43:63-64), Al-Maaidah (5:17), na An-Nisaa (4:171).

 

[8] Kauli Walizokhitilafiana Mayahudi Na Naswara Kuhusu Nabiy Iysaa (عليه السّلام) :

 

Baada ya Allaah (سبحانه وتعالى) Kubainisha hali ya ‘Iysaa mwana wa Maryam, jambo ambalo halina shaka, Allaah (سبحانه وتعالى) Anatuambia sasa kuwa makundi, yaani makundi ya upotofu kutoka kwa Mayahudi, Manaswara na wengineo katika daraja tofauti - wakakhitilafiana kuhusu Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام); ima kuvuka mipaka katika kumtukuza au kumkana na kumzushia.  Basi baadhi yao wakasema: “Yeye ni Allaah.” Na baadhi yao wakasema: “Yeye ni mwana wa Allaah.” Na baadhi ya wao wakasema: “Yeye ni tatu wa watatu.” Na baadhi yao kama Mayahudi, hawakumfanya ni Rasuli bali walimtuhumu kuwa ni mwana wa kahaba. Na kauli zote hizi ni baatwil na za uongo!

 

Maoni yao hayo ya baatwil yametokana na uvumi, ukaidi, ushahidi wa uongo na shubha na hoja zisizokuwa na nguvu.  Watu wote hawa wanastahiki onyo hili kali na ndipo Anasema (سبحانه وتعالى) Anasema:

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ ﴿٣٧﴾

“Basi ole wao wale waliokufuru na hudhurisho la Siku iliyo kuu kabisa.”

 

Yaani: Hudhurisho la Qiyaamah ambalo watahudhurishwa na kushuhudia wote; kuanzia wa mwanzo hadi wa mwisho, waja wa mbinguni na ardhini. Atakuweko Muumba na viumbe Alivyoviumba. Siku ambayo itajaa zilzala (mitetemeko ya ardhi) na viwewe. Na Siku ambayo itafanyika hesabu ya matendo. Juu ya hivyo, hiyo Siku itakuja kubainisha wazi kabisa yote waliyokuwa wakiyaficha na kuyafichua na waliyokuwa wakiyanyamazia (kuficha haki). [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[9] Nuwh Na Kizazi Kilobakia, Naye Ni Rasuli Wa Kwanza Ardhini Na Ni Baba Wa Wanaadam Baada Ya Aadam: Rejea Asw-Swaffaat (37:77).

 

[11]  Aayah Imekusanya Aina Tatu Za Tawhiyd:

 

‘Ulamaa wamesema kwamba Aayah hii imekusanya aina tatu za Tawhiyd kama ifuatavyo:

 

Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola Wake), na hii ni katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا

“Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake.”

 

Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada), na hii ni katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى): 

فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ

“Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake.”

 

Tawhiyd Asmaa Wasw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Yake Mazuri na Sifa Zake Tukufu Kamilifu), na hii ni katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

“Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?”

 

Hakuna Anayefanana Na Allaah (سبحانه وتعالى) Kwa Majina Yake Wala Kwa Lolote:

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا

Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?”

 

Naam! Hakuna anayefanana Naye kwa vyovyote wala kwa lolote, kwani Yeye Ni Mwenye Sifa za Pekee kama Anavyosema Mwenyewe Allaah (سبحانه وتعالى) :

 

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.”

 [Ash-Shuwraa (42:11)]

 

Na Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: Hakuna yeyote anayeitwa Ar-Rahmaan isipokuwa Allaah (تبارك وتعالى) na Jina Lake linatukuzwa [Tafsiyr Ibn Kathiyr] Na hakuna pia anayeitwa Allaah isipokuwa Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) Pekee!

 

[12] Hakuna Budi Kuupitia Moto Wa Jahannam:

 

Kauli hii wanaambiwa viumbe wote; wema wao na wapotofu wao, Waumini wao na makafiri wao, kwamba hakuna hata mmoja wao isipokuwa aupitie na aufikie moto. Hukmu ambayo Allaah (عزّ وجلّ) Ameilazimisha Nafsi Yake kutimizwa, na Akawatishia kwayo Waja Wake. Hapana budi kutokea kwake na hakuna kuiepuka.

 

Na ‘Ulamaa wamekhitalafiana katika maana ya neno al-wuruwd "الوُرُوْدُ", ambalo liko ndani ya Aayah hii kwa wizani wa “Ismu Faa’il” (وَارِدُ). Kundi la kwanza limesema kwamba maana yake ni kuufikia huo moto, kuhudhurishwa kwa viumbe wote mbele yake hadi kila mtu afazaike, kisha baada ya hapo Allaah Awaokoe Waumini wenye taqwa.

 

Ama kundi la pili, wao wamesema: Maana ya al-wuruwd ni kuingia ndani ya moto huo, lakini kwa Waumini utakuwa baridi na salama na amani kwao.

 

Ama kundi la tatu, wao wanaona kwamba maana ya al-wuruwd ni kupita juu ya Asw-Swiraatw ambayo chini yake kuna Jahannam, na watu watapita kwa kadiri ya 'amali zao. Kuna ambao watavuka kwa kadiri ya upepesaji wa jicho, na wengine watavuka kama upepo, na wengineo kama mwendo wa farasi, na wengineo kama mwendo wa kawaida wa vipando, na  wengineo watakuwa wanatembea haraka haraka, na wengine watakuwa wanavuka kwa mwendo wa kawaida wa kutembea, na wengineo watakuwa wanatambaa, na wengineo watanyakuliwa kisha watupwe motoni. Wote kulingana na uchaji wao (amali zao). [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

[13] Al-Baaqiyaatu Asw-Swaalihaatu: Mema Yanayobakia: Rejea Al-Kahf (17:46).

 

[15] Kumsingizia Na Kumshutumu Allaah (سبحانه وتعالى) Kwamba Ana Mwana!

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (قَالَ اللَّهُ: كَذَّبَنِي ابْنُ آدَمَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، وَشَتَمَنِي وَلَمْ يَكُنْ لَهُ ذَلِكَ، أَمَّا تَكْذِيبُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ إِنِّي لَنْ أُعِيدَهُ كَمَا بَدَأْتُهُ، وَأَمَّا شَتْمُهُ إِيَّاىَ أَنْ يَقُولَ اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا، وَأَنَا الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ أَلِدْ وَلَمْ أُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لِي كُفُؤًا أَحَدٌ))

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah Amesema: Binaadam amenikadhibisha, na wala hapaswi hilo! Na amenishutumu mja Wangu na wala hapaswi hilo! Ama kunikadhibisha kwake, amedai kuwa Sitoweza kumrudisha (kumfufua) kama alivyokuwa. Ama kunishutumu, ni kudai kuwa Nina mwana na ilhali Mimi Ni Asw-Swamad (Aliyekamilika Sifa za Utukufu Wake, Mkusudiwa wa haja zote) Ambaye Sikuzaa wala Sikuzaliwa na hakuna chochote kinachofanana na kulingana Nami.”   [Al-Bukhaariy]

 

Rejea Al-Baqarah (2:116), An-Nisaa (4:171), Al-Maaidah (5:17), (5:75), At-Tawbah (9:30).

 

[16] Mbingu Kuraruka Kutokana Na Kumzulia Allaah (سبحانه وتعالى) Ana Mwana:

 

Imaam As-Sa’diy:

 

Kauli Ya Allaah (سبحانه وتعالى):

تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾

“Zinakaribia mbingu kupasuka kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka!” [Maryam (19:90)]

 

Hili ni chukizo na fedheha kwa maneno ya watu wakaidi, wasio na shukrani ambao walidai kuwa Ar-Rahmaan Amejichukulia mtoto wa kiume. Ni kama walivyodai Manaswara kuwa Al-Masiyh, yaani Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  ni mwana wa Allaah, na Mayahudi kuwa ‘Uzayr ni mwana wa Allaah, na washirikina kuwa Malaika ni mabinti wa Allaah! Allaah Ametakasika na madai yao hayo na Yuko mbali nayo kabisa. [Tafsiyr As-Sa’diy]

 

Imaam Ibn Kathiyr:

 

Yaani: (Mbingu zinakaribia kupasuka) kutokana na Utukufu wake kwa Allaah zinaposikia kauli hii ya uovu itokayo kwa wanaadam. Sababu yake ni kuwa hizi (mbingu, ardhi n.k) ni viumbe vya Allaah na vimethibiti juu ya Tawhiyd Yake, na kwamba hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Hana washirika, Hana rika, Hana mtoto, Hana mwenzi na Hana mwenza, bali Yeye ni  Mmoja Pekee  Mkusudiwa wa haja zote, Hakuzaa wala Hakuzaliwa. [Al-Ikhlaasw]

 

Ibn ’Abbaas  (رضي الله عنهما) amesema kuhusu Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) :

تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾

“Zinakaribia mbingu kupasuka kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka!”

 

Hakika mbingu na ardhi na milima na viumbe vyote - isipokuwa wanaadam na majini - vinaogopa mno shirki. Na kutokana na U’adhwama wa Allaah,  viumbe hivi vinakaribia kutoweka Allaah Anapofanyiwa mshirika. Kama vile mshirikina hafaidiki na matendo yake mema kwa sababu ya kumshirikisha Allaah, kadhalika tunataraji kuwa Allaah Atawaghufuria madhambi wale waliompwekesha Allaah.  [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

Na Hadiyth kadhaa zimethibiti kuhusu umuhimu na uzito wa kumpwekesha Allaah na Neno zito la Tawhiyd na fadhila za Neno hili la:

 

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ

Laa ilaaha illa-Allaah

 

Bonyeza viungo vifuatavyo vyenye  faida tele:

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

Hadiyth: Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah - أحاديثُ عَنْ فضْل لا إلَهَ إلاَّ الله

 

Miongoni mwa Hadiyth hizo, ni hii ifuatayo: 

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرَيِّ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ الله (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ ((قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ يَا رَبِّ! عَلِّمْنِي شَيْئًا أَذْكُرُكَ وَأَدْعُوكَ بِهِ. قَالَ: قُلْ يَا مُوسَى: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ.  قَالَ يَا رَبِّ! كُلُّ عِبَادِكَ يَقُولُونَ هَذَا. قَالَ: يَا مُوسَى،  لَوْ أَنَّ السَّمَوَاتِ السَّبْعَ وَعَامِرَهُنَّ غَيْرِي وَالأَرَضِينَ السَّبْعَ فِي كِفَّةٍ،  وَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ فِي كِفَّةٍ، مَالَتْ بِهِنَّ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ))  رَوَاهُ ابْنُ حِبَّانَ وَالْحَاكِمُ وَصَحَّحَهُ.

Amesimulia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه):  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Muwsaa alisema: Ee Rabb wangu! Nifundishe kitu mahsusi kwangu ambacho kwacho nitakudhukuru na kukuomba duaa. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa!   Sema:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ 

Laa ilaaha illa-Allaah.  

 

Muwsaa akasema: Ee Rabb wangu! Waja Wako wote wanasema hivi. (Allaah) Akasema: Ee Muwsaa, lau kama mbingu saba na kila kilichokuwemo isipokuwa Mimi, na ardhi saba zikiwekwa katika kiganja cha mizani, na laa ilaaha illa-Allaah ikawekwa katika kiganja kingine cha mizani, basi laa ilaaha illa-Allaah itazishinda hizo.” [Ibn Hibaan, na Al-Haakim ameikiri kuwa ni Swahiyh]

 

Rejea Ash-Shuwraa (42:5), Al-Hashr (59:21).

 

Share