Mume Hapendi Kustarehe Na Mimi: Nyongeza Katika Majibu ya Swali La Kwanza

 

Mume Wangu Hapendi Kustarehe Na Mimi: Nyongeza Katika Majibu ya Swali La Kwanza

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalamu alykum.

 

Nimefurahi  sana kwa jawabu zenu  tatizo hili limeanza zamani tangu bada ya kuoana.

 

Mume Hapendi Kustarehe Na Mimi Anastarehe Nje Na Wanawake Nje

 

 

1)tatizo hilo  tangu baada ya kuaona 

2)ndio tumepata watoto  lkn kwakudra ya Allah Mwenyewe

3) tumeoana kijamaa 

4) yeye mwenyewe ndio alonitaka na mwenyewe nimemkubali.

5) hatukuwahi kupendana kimapenzi wala kukatana kimapenzi.

6) tokea awali ndio hivi hivi.

7) naishi mm na mume wangu tu lkn namshukuru Allah katupa watoto pia mume wangu hali miraa wala hatizami  film za ngono pia sikuwahi kumuona na habri hizo za kujichua. na hao wanawake sina uhakika  kama anfanya nao wla vipi  lkn nishawahi kuona msg  number za cmna pia kachat na mwanamke na kumstarehesha kwa maneno   kwa hiyo mm In Shaa Allaah nimo kusubiri na ntasubiri lkn nimechoka kifkra sijui kakusudia nini ikiwa mm hawezi kustarehe na mimi lkn huku anpenda wanawake.

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa dada yetu kwa nyongeza hizo. Lakini ibara nyingine zimekatwa katwa au hazieleweki ili kuweza kutoa nasaha za kina na za kutosheleza.

Hata hivyo, sisi hapa tunasema yafuatayo baada ya maelezo hayo:

 

 

1-Ikiwa tatizo hilo lilikuwa kuanzia muoane inaonyesha ana tatizo. Kwa hiyo, ni vyema uzungumze naye mumeo, kijamaa na kama mke wake ili muweze kwenda kuonana na daktari aliyebobea katika magonjwa ya kiume. Kwa kufanya hivyo, inawezekana ikapatikana dawa ya kuweza kumsaidia kuweza kustarehe nawe.

 

 

2-Huenda ikawa amesikia sifa zako au kwa sababu ya ujamaa alipendekewa akuoe kupitia kwa mzazi wake lakini yeye hakuwa na mapenzi nawe. Kwa kuwaridhisha wazazi wake alifanya hivyo ndivyo hahisi kabisa kustarehe nawe.

 

 

3-Inawezekana kuwa kwa kuwasiliana na mwanamke au wanawake wengine akawa anaona aoe mwingine au anaona kwa kufanya hivyo utataka talaka ili isionekane yeye ndio hakutaki. Kwa hiyo, akapata fursa ya kumuoa amtakae kwa ridhaa yake bila kuelekezwa na mtu mwingine.

 

 

4-Tatizo kama hilo huwa bila shaka linashosha kifikra, kiakili, kifiziolojia na ikiwa shida hiyo haitatatuliwa mapema huenda ikakufishika sehemu mbaya sana.

 

 

Kwa tatizo lilivyo tunaona unaweza kufanya yafuatayo:

 

 

a-Ukae na mumeo kama wanandoa na mzungumze kiutu uzima hilo tatizo kwa uwazi na bila kuficha. Ikiwa kila mmoja atakuwa wazi kwa mwenziwe huenda suluhisho ikapatikana kwa usahali kabisa

 

 

b-Ikiwa hatua hiyo ya kwanza haikuzaa natija yoyote, bila shaka itakuwa muhimu sana kwa wazazi wa kila upande waje katika mkutano wa kutaka upatanishi na tatizo hilo sugu baina yenu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)   Ameahidi kuwa lau kila upande utakuja katika kikao hicho kwa niyya nzuri, ikhlaasw na kutaka upatano basi suluhisho la kudumu litapatikana. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾

Na mkikhofu mafarikiano baina yao wawili, basi pelekeni mwamuzi kutoka watu wa mume na mwamuzi kutoka watu mke. Wakitaka sulhu Allaah Atawawafikisha baina yao.  Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [An-Nisaa: 35]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa suluhu Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo. Na mkifanya ihsaan na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika [An-Nisaa: 128]

 

 

c-Ikiwa hakuna suluhisho lolote basi itabidi mutengane na jambo hilo litakuwa bora kwa kila mmoja. Kufanya hivyo, itampatia fursa kila mmoja kuweza kupata mwendani mwengine ambaye ataweza kuridhiana naye kwa kiasi kikubwa zaidi. Hili litafanyika tu ikiwa njia nyingine hazikufaulu.

 

 

Tunakuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akuwafikie na kukuondolea tatizo hilo kwa wakati muafaka kabisa.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share