Shaykh Fawzaan: Usisuhubiane Na Watu Wa Bid'ah

 
Usisuhubiane na Watu Wa Bid'ah

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 
 
Shaykh Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) aliulizwa:
 
 
"Kuna mtu tuko naye kazini, anakubali sherehe za Mawlid na anayatetea, na anashikilia hilo; je, nimhame kwa ajili ya Allaah au hapana? Nifanye nini? Na Jazaakum Allaahu khayra.
 
 
Akajibu Shaykh (Hafidhwahu Allaah):
 
"Kusherehekea Mawlid ya Nabiy ni bid'ah. Na anayeyakubali na kuyapendekezesha, basi huyo ni mtu wa bid'ah (Mubtadi'). Na akishikilia msimamo wake huo na hakubali nasaha na akaendelea kuyatangaza na kuwapendezeshea watu hilo, basi mtu huyu inapasa kumhama kwa sababu ni mzushi (Mubtadi'). Mzushi haifai kusuhubiana naye."
 
 
[Al-Multaqaa Min Fataawa Ash-Shaykh Al-Fawzaan]
 
 
Share