Supu Ya Boga Na Figili Mwitu Celery

Supu Ya Boga Na Figili Mwitu Celery

Vipimo

Boga dogo katakata vipande vidogodogo - 1

Siagi - 1 kijiko cha supu

Figili mwitu (celery) - 2 Miche

Kidonge cha supu cha nyama ng’ombe au kuku - 1

Maziwa   - ½ Kikombe

Maji   - 2 – 3 Vikombe

Chumvi - ¼ kijiko cha chai

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Ndimu - ukipenda

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

1. Weka siagi katika sufuria, kaanga vipande vya maboga pamoja na figili mwitu.

2. Chambua kidonge cha supu uchanganye, kaanga mpaka iwe rangi ya kahawa isiyokoza (light brown)

3. Tia maji iache ichemke mpaka iwive, kisha saga katika mashine (blender)

4. Rudisha katika sufuria, tia maziwa, ikiwa nzito ongezea maji.

5.Tia chumvi,  pilipili manga na ukipenda ndimu kidogo tu.

6. Epua ikiwa tayari.

 

Figili Mwitu                                                                 Boga

                        

                                     

 

 

 

 

Share