Sharbati Ya Boga Ya Mdalasini

 

Sharbati Ya Boga Ya Mdalasini

(Kupata takriban gilasi  7 )

 

Vipimo

Boga lilopikwa - 2 vikombe

Maziwa ya kibati (evaporated milk) - 1 kikombe

Maziwa ya kawaida - 3 au 4 vikombe

Mdalasini wa unga - 1 kijiko cha chai

Sukari - 1/3 (robo) kikombe

Hiliki - ½ kijiko cha chai

Barafu vipande vipande - Kikombe 1

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Menya na kata boga vipande kisha weka katika sufuria. Weka maji  kidogo ya kutosheleza kuwivisha.
  2. Funika uchemshe hadi liwive
  3. Tia katika mashine ya kusagia (blender)
  4. Tia vitu vilobakia upige vizuri. Onja sukari uongeze upendavyo.
  5. Mimina katika gilasi ikiwa tayari

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kufurahika)

 

 

Share