Fir'awn Na Mkewe Kuhusu Maingiliano Yao

SWALI:

Firaauuni [l.a] aliwahi kumwingilia mkewe?

 JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Fir’auni alimwingilia mkewe siku alizojaaliwa kumwingilia lakini wakati walipotunukiwa kumuokota na kumlea Nabii Musa a.s. hawakuwa na mtoto. Baada ya mwanamke huyo kusilimu na kumfuata Nabii Musa ‘alayhi ssalam. na kumkanusha mumewe aliteswa na yumkini kuwa baada ya hapo hawakuonana kimwili. Na jambo lenyewe si muhimu katika Imani hata ikiwa alimuingilia au hakumuingilia. Kujua hilo halitatuongezea chochote katika Imani yetu.

Na Allah anajua zaidi

 

 

Share