Shurba Ya Oats Ya Kukobolewa (Jariysh) Kwa Nyama Mbuzi

Shurba Ya Oats Ya Kukobolewa (Jariysh) Kwa Nyama Mbuzi

Vipimo

Nyama mbuzi - ½ kilo

Oats zilokobolewa (Jariysh) - 1 ¼ kikombe

Vitunguu - 2

Nyanya/tungule - 2

Samli - 2 vijiko vya supu

Kidonge cha supu - 1

Chumvi - kiasi

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai                                  

Kotimiri iliyokatwakatwa - 1 kikombe cha chai           

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Roweka oats kiasi  saa moja au zaidi
  2. Chemsha nyama  kwa maji ya kutosha ili ibakie supu kiasi vikombe 7.
  3. Toa nyama, chambua mifupa unyambue nyama au ikatekate (chopped)
  4. Weka sufuria katika moto, weka samli, kaanga vitunguu hadi vilainike na kubadilika rangi kisha weka nyanya.
  5. Weka nyama, chumvi pilipili manga, kidonge cha supu changanya vizuri.
  6. Tia supu ufunike upike kwa moto mdogo mdogo kiasi saa moja.
  7. Unaweza kuongeza kidogo maji ya moto ikitokea kuwa nzito sana.
  8. Weka kotmiri, ikiwa tayari.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 Oats Zilokobolewa (Quacked oats/jariysh)

 

 

 

 

 

Share