Maandazi ya Alkarii (Baluchi)

Maandazi ya Alkarii (Baluchi)

Vipimo

Unga -  2 vikombe vikubwa (mugs)

Baking powder -  ½ kijiko cha chai

Siagi - 2 vijiko vya supu

Sukari - ¼ mug

Mayai -  2

Maziwa au maji -   ½ mug

Hiliki -  2 chembe saga

Mafuta ya kukaangia -  ½ litre

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Chunga unga, weka baking powder, hiliki, siagi, vuruga mpaka uchanganyike vizuri
  2. Piga mayai katika kibakuli.
  3. Tia sukari changanya, weka mayai changanya, kisha tia maziwa au maji kanda  mpaka uwe laini. Ukiwa mgumu ongeza maji kidogo.
  4. Kata vidonge, kisha sukuma kila kidonge peke yake au sukuma katika katikati ukipenda
  5. Kaanga kwenye karai katika mafuta ya moto mpaka yawe rangi ya hudhurungi huku ukigeuza.
  6. Epua uchuje mafuta, yakiwa tayari. 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share