Buns Za Nyama Ya Kusaga (Aina Ya 1)

Buns Za Nyama Ya Kusaga (Aina Ya 1)

Vipimo Vya Nyama
 
Nyama ya kusaga - 1/2 Kilo
Pili pili manga - 2 Vijiko vya chakula
chumvi - kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha chakula
Ndimu - 2 vijiko vya chakula
Bizari mchanganyiko - 1 Kijiko cha chakula
Pilipili boga - Nusu
 
Vipimo Vya Kukanda Unga Wa Mkate
Unga wa ngano - 3  vikome vikubwa
chumvi - 1  kijiko  cha chakula
Hamira - 2 vijiko vya chakula
Samli au siagi - 3 vijiko vya chakula
Maji au nazi - kiasi ya kukandia
 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
  1. Kausha nyama yako kwa vitu vyote isipokuwa pilipili boga, tia     mwisho karibu na nyama kukauka. Weka nyama pembeni.
  2. Changaya unga pamoja na vitu vyote, uvuruge vizuri kwa maji ya  vuguvugu (au ukipenda nazi)  na ukande ulainike.
  3. Ukilainika tengeneza madonge ya kiasi, tia nyama ndani yake kwa kuteka na   kijiko.
  4. Panga kwenye treya, yaache madonge yaumuke.
  5. Yakishaumuka yachome (bake) katika moto wa 300 au 350 kwa muda wa dakika 20 takriban au mpaka yabadilike rangi kidogo na yawive.
  6. Yakishawiva, epua na upake mafuta kidogo juu yake ili yalainike na tayari kuliwa. 

 

Share