Vitumbua Vya Mayai Vidogodogo -1

Vitumbua Vya Mayai Vidogodogo -1

 

Vipimo

Mchele - 2 mugs

Hamira -  2 vijiko vya chai mfuto

Sukari -  ¼ robo magi takriban

Tui la nazi zito - 2 mugs

Maziwa ya unga - 2 vijiko vya supu

Mayai - 2

Hiliki -  ½ kijiko cha chai

Vanilla - 1 kifuniko cha chupa

Mafuta ya kupikia - 1 kikombe takriban

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Roweka mchele masaa 5 kiasi au zaidi yake
  2. Chuja mchele kisha weka katika blender. Tia nazi mug 1 kwanza piga usagike vizuri.
  3. Tia vitu vilobakia uendeleee kusaga vizuri.
  4. Funika uumuke. Kisha pika katika chuma cha vishimo vidogodogo kwa kuweka mafuta kiasi nusu kijiko cha kulia katika kila kishimo.
  5. Epua vichuje mafuta. Kisha weka katika tissue ya jikoni vizidi kuchuja mafuta. Panga katika sahani vikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share