Shaykh Fawzaan: Ramadhwaan: Alama Za Kukubaliwa 'Amali Katika Ramadhwaan

 

Alama Za Kukubaliwa 'Amali (Matendo) Katika Ramadhwaan

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

 

"Miongoni mwa alama za kukubaliwa (matendo) katika Ramadhwaan na katika miezi mingine (inayofuatia), ni kufuatishia jema kwa jema.

 

Basi pindi inapokuwa hali ya Muislamu baada ya Ramadhwaan ni njema, huwa anazidisha mema na matendo mazuri. Na hii ni dalili ya kukubaliwa

(mja matendo yake).

 

Ama hali ikiwa kinyume; (mtu) akafuatishia mema kwa (kufanya) maovu; (yaani) pindi Ramadhwaan inapoondoka, akafuatishia kwa kufanya maovu na kupuuzia 'amali na kuwa kinyume na utiifu kwa Allaah, basi hii ni dalili ya kutokubaliwa (matendo yake)."

 

 

[Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 119]

 

 

 

 

Share