Imaam Ibn Taymiyyah: Utaratibu Kumhusu Imaam Anapomaliza Swalaah

Utaratibu Kumhusu Imaam Anapomaliza Swalaah

Imaam  Ibn Taymiyyah (Rahimahu-Allah)

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Inampasa Maamuma asinyanyuke (baada ya Swalaah) hadi atakapomaliza Imaam; yaani atakapohama kugeuka kutoka alipokuwa akielekea Qiblah. Na wala haimpasi Imaam kukaa na kuelekea Qiblah baada ya kutoa Salaam ila kiwango (kidogo tu cha kutosha) kufanya Istighfaar mara tatu, na kusema ‘Allaahumma Anta As-Salaam wa minka As-Salaam tabaarakta yaa Dhaal-Jalaali wal-Ikraam’.

 

Na pindi anapogeuka Imaam (kugeukia watu baada ya Swalaah), basi yule mwenye kutaka kusimama (kuondoka) asimame, na mwenye kupenda kukaa na kumdhukuru Allaah, basi na afanye.”

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa, mj. 22. Uk. 505]

 

Share