Imaam Ibn Taymiyyah: Tawassul Na Adhkaar Zisizokuwa Za Sunnah Hazipasi Kufundishwa Wala Kuzisoma

 

Tawassul Na Adhkaar Zisizokuwa Za Sunnah Hazipasi Kufundishwa Wala Kuzisoma

 

 Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

“Hapana shaka kwamba adkhaar na du’aa ni ‘ibaadah bora kabisa, na ‘ibaadah ni jambo mojawapo ambalo hakuna upenyo wa mtu kuleta rai zake. Inatupasa tufuate aliyotufunza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na si matamanio yetu au uzushi. Du’aa na adhkaar za Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni bora zaidi kuliko zozote nyinginezo. Na mwenye kuzifuata atabakia salama na kutenda yaliyo sahihi, na manufaa na matokeo mazuri atakayochuma ni mengi hata hayaelezeki.

 

Du’aa na adhkaar zozote nyinginezo zinakuwa ni haramu au makruhu kwani zinaweza kuhusiana na shirk japokuwa watu wengi hawatambui hilo. Maelezo yake ni marefu mno kuyaelezea hapa.

 

Mtu hana haki kufundisha watu du’aa au adhkaar zozote zisizokuwa katika Sunnah, au kuzifanya kuwa ni ‘ibaadah ya mazoea ambayo anategema watu kuifanya kama wafanyavyo Swalaah tano. Huu ni uzushi katika Dini ambao Allaah Hajautolea idhini. Ama kupanga uradi au kusoma kwa kudumisha adhkaar ambazo hazikuamrishwa katika shariy’ah, ni jambo lisiloruhusiwa.

 

Du’aa na adhkaar zilizoamrishwa katika shariy’ah, ni bora zaidi kwa yeyote kuzitaraji na kuzipata na hakuna anayezipuuza kwa kufadhilisha zilizo mpya za uzushi, au adhkaar za uzushi isipokuwa ambaye ni mjinga au mtendaji makosa.”

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawa (22/510/511)]

 

 

Share