Habbat Sawdaa: Manufaa Yake - 3

 

Habbat Sawdaa: Manufaa Yake - 3

 

Imekusanywa Na: Iliyaasah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

 

  عن أبي هريرة رضي الله عنه أنه سمع رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «في الحَبَّةِ السوْدَاءِ شِفَاءٌ من كل دَاءٍ إلاَّ السَّام

Amesimulia Abu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akisema: “Katika Habbat-Sawdaa kuna Shifaa (Poza) ya kila maradhi isipokuwa sumu.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Asidi (Acidness)

Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.  

 

 

 

Uvimbe Wa Tumbo

Chukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu unywe; utaona nafuu kubwa kwa uwezo wa Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى).

 

 

Maradhi Ya Macho

Pakaza  mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope. Fanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha vuguvugu au katika juisi ya karoti.

 

 

Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)

Chukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, kisha changanya  katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; utakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

 

 

 

Kichocho (Bilharziasis)

Tafuna  Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni. Unaweza  kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Endelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Utapata nguvu na nishati kwa uwezo wa Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى).

 

 

Kutoa Wadudu Tumboni

Kula sandwichi ya vitu vifuatavyo:

Kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash). Kunywa asubuhi kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.

 

 

 

Utasa

Chukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, utakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae utafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi kwa uwezo wa Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى) utapona.

 

 

Tezikibofu (Prostate gland)

Jipakaze mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na jipake chini ya korodani (sehemu ya siri) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.

 

 

 

Pumu (Asthma)

Kula Habbat-Sawdaa ilosagwa kwa asali, au tumia mafuta ya Habbat-Sawdaa na asali asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.

 

 

 

Kidonda

Changanya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. utakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae unywe gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.

 

 

 

Saratani (Cancer)

Pakaza mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila unapomaliza  kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Endelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.

 

Au Unaweza kuchanganya unga wa Habbat-Sawdaa na kitunguu thomu (saumu) kilosagwa au kukunwa na changanya na asali uwe unakula kila siku kijiko kimoja cha chai kila kabla ya kula chakula kikuu Yaani mara tatu kwa siku.

 

 

 

Nguvu Za Kiume

Chukua  unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja uchanganye ndani ya mayai saba ya kienyeji. Fanya hivyo siku baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi hata kama una miaka 120 atapata nguvu za barobaro!

 

Udhaifu kwa Ujumla

Chukua unga wa Habbat Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari (ambergris) ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote utavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu uwe unakula kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.

 

 

Kuleta Hamu Ya Kula

Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.

 

 

 

Kutibu Ulegevu Na Uvivu

Kabla ya kula chakula, kunywa juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Endelea hivyo kwa muda wa siku kumi.  Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.

 

 

 

Nishati Akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi

Chemsha nanaa (mint leaves), uichanganye na asali na uingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; unywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi.

 

 

 

 

Share