Al-Lajnah Ad-Daaimah: Haijuzu Kufupisha Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Maandishi

 

Haijuzu Kufupisha Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 Katika Maandishi  

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Swali liliulizwa kuhusu kupifisha kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Jibu:

 

 

"Sunnah ni kuandika ibara kikamilifu (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwani hivyo ni kama du’aa, na du’aa ni ‘Ibaadah (ikiwa kuandika) kama ilivyo katika kutamka. Hivyo kufupisha kutumia herufi (Swaad ص ) au herufi kama (Swaad-Laam-‘Ayn-Miym) sio du’aa wala ‘ibaadah  ikiwa imetajwa katika kutamka au maandishi. Kwa sababu kufupisha huko hakukutumiliwa na karne tatu za mwanzo ambazo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amezishuhudia ubora wake.”

 

[Fataawaa Al-Lajnat Ad-Daa'imah Namba 18770 (12/208-209) – Kamatia Ya Kudumu Ikiongozwa na Shaykh bin Baaz]  

 

 

Tanbihi:  Aghlabu ya watu katika jamii hufupisha kwa kuandika (S.A.W)  yaani “Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam” au kwa kingereza (P.B.U.H) yaani: “Peace be upon him.”  Basi haijuzu kufupish kwa aina yoyote ile.

 

 

 

Share