Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-'Abbaad: Maulidi: Kula Chakula Kinachoandaliwa Kwa Ajili Ya Bid’ah

 

Kula Chakula Kinachoandaliwa Kwa Ajili Ya Bid’ah Kama Ya Mawlid

 

Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com 

 

 

SWALI:

 

Je, inafaa kula chakula cha watu wa bid’ah kwa kujua kwamba wanaandaa chakula hicho kwa ajili ya bid’ah hiyo, kama kuandaa chakula cha mawlid ya Nabiy?

 

 

JIBU:

 

Ni waajib kuwatanabahisha kwamba wanavuka mipaka katika bid’ah, na kwamba wasifanye yaliyoharamishwa. 

 

Na mtu hatakiwi kula chakula kinachoandaliwa kwa ajili ya  mambo ya bid’ah na mambo yaliyoharamishwa. 

Kwa hiyo hapasi mtu kutumia chakula hicho bali inampasa atanabahi na atahadhari kuingia katika mambo hayo yaliyoharamishwa.

 

 

[Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad

 

 

Share