Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kumuita Aliyefariki ‘Marehemu’ Haijuzu

Kumuita Aliyefariki ‘Marehemu’ Haijuzu

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

Je, Inafaa Maiti Kuitwa Marehemu?

 

SWALI:

 

Je, inafaa kumtaja mtu aliyefariki kwa kusema Marehemu (ambaye amerehemewa) fulani  au fulani, kama mfano kusema:  “Marehemu baba yangu?”

 

 

JIBU:

 

Haifai kabisa kumtaja aliyefariki ‘Marehemu’ au ‘Marhuwm’ bali atajwe: “Fulani Allaah Amrehemu.”  Hivi kwa sababu kusema ‘Marehemu’ ni sawa na kusema kuwa aliyefariki ameshateremshiwa rahmah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na hali hakuna mtu yeyote anayejua jambo hili isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq. Swalaah na salaam kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba zake.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-‘Ilimiyyah, Swali Namba (6360)]

 

 

Tanbihi:

Kuna Wanachuoni kama Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) wanaoona inafaa kumuita maiti 'Marehemu', lakini kauli yenye nguvu ni hiyo juu ya Al-Lajnatud-Daaimah.

 

 

Share