Imaam Atw-Twabariy: Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah Hayakuumbwa

 

 Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah Hayakuumbwa

 

Imaam Atw-Twabariy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 Imaam Atw-Twabariy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Qur-aan ni maneno ya Allaah na Tanziyl yake (yaani Wahyi wake), haikuumbwa katika hali yoyote inaweza kuwa imeandikwa au wakati ilipokuwa ikisomwa, katika mahali popote inaposomwa, kama jinsi ilivyopatikana katika mbingu au juu ya ardhi, hata hivyo inaweza kuwa imehifadhiwa kama ilivyoandikwa katika Lawhul-Mahfuwdhw au katika nakala za watoto wa shule za Qur-aan, au ilipoandikwa juu ya jiwe na kuandikwa juu ya karatasi au majani, kama kuihifadhi katika moyo, au kusemwa na ulimi. Yeyote yule atakayesema kinyume na haya, au akadai kuwa Qur-aan ambayo tunaisoma na ndimi zetu, na ambayo tumeandika katika Mswahafu, au ambaye ataamini katika moyo wake au ambaye ataficha aina ya imani kama hiyo katika moyo wake, au ambaye atakiri kwa ulimi wake, basi yeye ni kafiri ambaye damu na mali yake ni halali na ambaye atakuwa mbali na Allaah na Allaah yuko mbali naye.” [Atw-Twabariy, Swarihus-Sunnah, 24-25].

 

 

Share