Imaam Al-Albaaniy: Bali Atakuadhibu Kwa Kwenda Kinyume Na Sunnah

 

Bali Atakuadhibu Kwa Kwenda Kinyume Na Sunnah

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

 

“Amesimulia Al-Bayhaqiy kwa sanad iliyo sahihi kutoka kwa Sa’iyd bin Musayyib kwamba alimuona mtu akiswali zaidi ya rakaa mbili baada ya kuchomoza jua la Alfajiri, akikithirisha ndani ya Swalaah hiyo kurukuu na kusujudu; akamkataza.

Yule mtu akasema:

“Ee Abaa Muhammad, (Unanikataza kwani) Ataniadhibu mimi Allaah kuswali (hii Swalaah)?

Akajibu (Sa’iyd bin Musayyib):

“Bali (Allaah) Atakuadhibu kwa kwenda kinyume na Sunnah (kwa sababu hiyo Swalaah kwa mtindo huo hakuifunza Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).”

 

(Anasema Imaam Al-Albaaniy) Na haya ni katika majibu yenye ukomo wa kuvutia ya Sa’iyd bin Musayyib (Rahimahu Allaahu Ta’aalaa), nayo ni silaha yenye nguvu kwa wazushi ambao wanapendezesha bid’ah zao nyingi kwa kuyapa majina kuwa ni katika Adhkaar na ni katika Swalaah, kisha wanawapinga Ahlus-Sunnah kwa sababu wanawakataza wao uzushi huo, na wanawatuhumu (Ahlus Sunnnah) kuwa wanawakataza kufanya Adhkaar na kuswali!!

Nao kiuhakika wanachowakataza (hao wazushi) ni kupingana nao na kukhalifu kwao Sunnah katika Adhkaar na katika Swalaah na mengine mfano wa hayo.

 

 

[Irwaa-u Al-Ghaliyl Fiy Takhriyj Ahaadiyth Manaar A-Sabiyl, mj.2, uk.236]

 

 

Share