Imaam Al-Albaaniy: Miongoni Mwa Sababu Ya Kuangamia Ummah Ni Kutokana Na Wahadhiri Wa Visa

 

Miongoni Mwa Sababu Ya Kuangamia Ummah Ni Kutokana Na Qusswaasw (Wahadhiri Wanaotilia Himma Visa (Vya Uongo) Katika Mawaidha Yao)

 

Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

Amesema Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah):

 

Kuhusu Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Hakika Bani Israaiyl wameangamia kutokana na kutoa kwao visa.” [Swahiyh Al-Jaami’ (2045)]. 

 

“Hakika sababu ya kuangamia kwao ni vile kutilia himma kwao mawaidha yao kwa visa na hikaya bila ya Fiqh na ‘ilmu ya manufaa ambayo itawajulisha watu kuhusu Dini yao, wanawabebesha watu hayo kwa (kuwahamasisha kwa hivyo visa) kufanya matendo mema. Na kwa kufanya kwao hayo, wakaangamia. Na hili ndio jambo la wengi miongoni mwa Quswaasw (wapiga visa vya uongo) wa zama zetu ambao wingi wa mazungumzo yao kati mawaidha yao, ni (visa) vya israailiyyaat na vilainisha moyo na Usufi.

 

Tunamuomba Allaah Atulinde na Atuhifadhi na Atusalimishe.

 

 

[As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/248)]

 

 

Share