Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hukmu Ya Mwenye Kuswali Bila Ya Wudhuu

Hukmu Ya Mwenye Kuswali Bila Ya Wudhuu
 
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
 
 
 
SWALI:
 
Nilighafilika kuwa sina wudhuu na nikaswali, baada ya kumaliza Swalaah yangu nikakumbuka kuwa sikuwa na wudhuu. Je, natakiwa kurudia Swalaah yangu?
 
 
JIBU:
 
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala).
 
Ndio, ikiwa mtu amesahau na akaswali hali ya kuwa hana wudhuu basi ni lazima arudie Swalaah yake, kwa sababu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) amesema:
“Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Hakubali Swalaah yoyote ikiwa mtu atakuwa hana wudhuu (atavunja wudhuu), mpaka atakapokuwa na wudhuu (ndiyo Swalaah yake itakubaliwa).” [Imekusanywa na Al-Bukhaariy kutoka katika Hadiyth iliyosimuliwa na Abuu Hurayrah]
 
Hii ni tofauti na mtu mwenye najisi katika nguo zake na akasahau (kuisafisha). Hatakiwi kurudia Swalaah yake, kwa sababu Jibriyl (‘Alayhis-Salaam) alimuendea Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) wakati alipokuwa akiswali, na akamwambia kuwa kuna uchafu kwenye viatu vyake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi sallam) alivivua na kuendelea kuswali.
[Imesimuliwa na Ahmad katika musnad yake kutoka katika Hadiyth ya Abuu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu ‘anhu)].
 
Hadiyth hiyo ni ushahidi kuwa akiwa mtu hajui kuwa anayo najisi basi haimpasi kurudia Swalaah yake, na inatumika pia kwa yule ambaye amesahau kuwa alikuwa na najisi.
 
 
[I'laam Al-Musaafiriyn Bi Ba'dhw Aadaab Wa Ahkaam As-Safar Wa Maa Yakhusw Al-Mallaahiyn Al-Jawwiyyiyn, uk. 12]
 
 
Share