Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Ramadhwaan: Mwenye Deni Lazima Ailipe Kabla Ya Ramadhwaan Nyingine Kuingia

 

Aliyekuwa Na Deni La Ramadhwaan Iliyopita

Ni Lazima Ailipe Kabla ya Ramadhwaan Nyingine Kuingia

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

"Hairuhusiwi kuahirisha ulipaji deni wa Swawm (ya Ramadhwaan iliyopita) hadi ikaingia Ramadhwaan nyingine bila udhuru (unaokubalika kishariy'ah).

Hiili ni kwa sababu ya maelezo ya mama wa Waumini 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): 'Nilikuwa na deni la Swawm ya Ramadhwaan na sikuweza kulipa ila katika Sha'baan.' [Al-Bukhaariy]

 

 

[Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 59]

 

Share