Kumwakilisha Mtu Kwenye Ndoa

 

Kumwakilisha Mtu Kwenye Ndoa

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

assalaamu alaykum je, nini hukumu ya kuwakilishana katika kuoa, yaani kuoa kwa niaba ya ndugu yako; ikiwa inafaa, je ni zipi taratibu zake?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Wa 'Alaykumus Salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh

 

Kukiwa na dharura ya kukosekana kwako kwenye kufunga ndoa, unaweza kutoa idhini yako ima kwa maandishi au kwa njia ya simu inayothibitisha ni wewe na Walii (baba wa mke au babu au kaka) akawepo na mashahidi wawili na mahari.

 

Tambua kuwa lazima awepo Walii wa mwanamke unayetaka kumuoa, kukosekana Walii kunaifanya ndoa isiwe sahihi; yaani batili.

 

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Hakuna ndoa bila Walii.” [Ibn Maajah, At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd na Al-Albaaniy kasema ni sahihi]

 

Lakini, ni bora zaidi kusubiri mwenyewe upatapo hiyo nafasi ya kwenda kufunga ndoa mwenyewe kwa sababu nyingi muhimu na zenye faida kwako wewe mwenyewe kuliko kumwakilisha mtu.

 

Kuwepo kwako utapata Sunnah nyingi za jambo hilo, kuanzia kufungishwa ndoa na kuitikia mwenyewe kukubali kwako kumuoa huyo mke, vilevile utapata kufurahi na pia kuwa na wasaa wa kuwa na mkeo na kufanya yale ambayo mume na mke wanayafanya ya starehe na furaha, na mengine mengi katika siku hiyo adhimu ya furaha.

 

Kwa faida zaidi, bonyeza kiungo hapa chini usome:

 

Yanayopasa Na Yasiyopasa Kutendeka Katika Ndoa

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

Share