Mishkaki Ya Kuku Kwa Bizari Mchanganyiko Na Hardali

 

Mishkaki Ya Kuku Kwa Bizari Mchanganyiko Na Hardali  

 

Vipimo  

 

Kuku kidari – kilo 1   

Bizari mchanganyiko – 1 kijiko cha kulia

Sosi ya hardali (Mustard sauce) – 1 kijiko cha kulia

Chumvi kiasi

Mtindi – ½ kikombe

Mafuta – vijiko 2 vya kulia

Vitunguu – 2

Pilipili boga la kijani – 2   

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Osha kidari cha kuku uchuje maji. Kisha katakata vipande uweke katika bakuli.
  2. Katika kibakuli kidogo, changanya bizari, hardali, mtindi, chumvi na mafuta uchanganye vizuri.
  3. Mimina katika kuku uchanganye vizuri kabisa. Weka katika friji akolee viungo kwa muda wa saa au zaidi.
  4. Katakata vitunguu na pilipili boga vipande vikubwa kiasi vya kuchomekea katika mishkaki.
  5. Chomeka vipande  vya kuku katika vijiti yva mishkaki ukiweka baina yake vipande vya vitunguu na pilipipili boga.
  6. Weka katika treya kisha choma (grill) katika mkaa au oven.
  7. Ikishawiva epua upange katika sahani.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share