Pweza Wa Kukaanga

   Pweza Wa Kukaanga  

  

Vipimo  

Pweza  - 1 Kilo

Mafuta -  ½ kikombe

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Tangawizi mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Kitunguu saumu (thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Masala ukipenda - 1 kijiko cha supu  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Osha pweza kisha mkatekate   
  2. Mtie viungo vyote ulotayarisha  na   chumvi 
  3. Muache nusu saaa akolee viungo 
  4. Mtie ndani ya sufuria bila maji mfunike kisha weka jikoni, atatumbuka maji mwenyewe kwa moto wa kiasi paka awe rangi ya damu yam zee (maroon) 
  5. Akishawiva kwa rangi hiyo basi sasa mwaga maji yote,chukua pweza pekee weka kwenye bakuli au sahani 
  6. Weka karai au kikaango (frying pan) motoni tia mafuta  acha kwa muda wa dakika tano hivi mafuta  yapate moto. 
  7. Mimina pweza kwenye karai aacha wakaangike paka wabadilike ukiwageuza geuza kila baada ya muda wa dakika kumi hivi.  Pweza tayari kwa kuliwa   kwa ugali au muhogo 

Kidokezo:   

Unaweza kumwagia masala kiasi baada ya kukaanga kama picha inavyo onyesha.

 

 

Share