Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hajj: Anayetia Niyyah Kuchinja Asikate Nywele, Kucha

Anayetia Niyyah Kuchinja Asikate Au Kunyoa Nywele Au Kukata Kucha

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

‘Ulamaa wa Al-Lajnah Ad-Daaimah wamesema:

“Imewekewa Shariy'ah kwa yule mwenye kutaka kuchinja pindi unapoandama mwezi wa Dhul-Hijjah, asitoe chochote katika nywele zake au kucha zake au ngozi yake mpaka amalize kuchinja.

Dalili ni kutoka kwa Al-Jamaa’ah isipokuwa Al-Bukhaariy (Rahimahumu-Allaah): Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “

 

 إذا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الحجّة وَأَرَادَ أحدكم أَنْ يُضَحِّيَ فَلْيُمْسِكْ عن شَعْرِهِ وَأَظْفَاره

((Pindi mkiona mwandamo wa mwezi wa Dhul-Hijjah na mmoja wenu akitaka kuchinja, basi azuie nywele zake na kucha zake))

 

Na lafdhi ya Abuu Daawuuwd, Muslim na An-Nasaaiy:

 

مَنْ كَانَ لَهُ ذَبْحٌ يَذْبَحُهُ فَإِذَا أَهَلَّ هِلالَ ذِي الْحِجَّةِ فَلا يَأْخُذَنَّ مِنْ شَعْرِهِ وَلا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا حَتَّى يُضَحِّيَ  

((Ikiwa kuna mwenye mnyama wa kuchinja, basi utakapoandama mwezi wa Dhul-Hijjah asitoe chochote katika nywele zake au kucha zake mpaka achinje))

 

Hukmu hiyo ni kwa mwenye kuchinja mwenyewe au hata ikiwa amewakilisha mtu amchinjie. Lakini mwenye kuchinjiwa (mf. wana familia; mama au watoto) yeye haimuwajibikii hukmu hii kwa kuwa hakuna dalili ya hilo.

Wala haiitwi hiyo ni Ihraam, kwani Muhrim ni yule ambaye anaingia katika Ihraam kwa ajili ya Hajj au ‘Umrah au zote mbili.”

 

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (11/397-398)]

 

 

Share