Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hajj: Nani Wa Kujizuia Nywele Na Kucha Katika Kuchinja (Udhwhiyah)?

Nani Wa Kujizuia Kukata Nywele Na Kucha Katika Kuchinja (Udhwhiyah)?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Kuhusu Hadiyth hii:

"Anayetala kuchinja au kumwakilisha mtu kumchinjia, kutokea siku ya kwanza ya Dhul-Hijjah, asiondoshe (asikate) chochote katika nywele zake, wala ngozi yake, wala kucha zake hadi atakapochinja."

Je, hukmu hii inawajibika kwa watu wote wa nyumbani kwake, wakubwa wao na wadogo wao au wakubwa wao tu?

 

 

JIBU:

 

Hatujui lafdhi ya Hadiyth kama aliyoulizia muulizaji. Lafdhi tunayojua iliyothibiti kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni ambayo wameipokea Al-Jamaa’ah isipokuwa Al-Bukhaariy:

Imepokelewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “

 

 إذا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الحجّة وَأَرَادَ أحدكم أَنْ يُضَحِّيَ فَلْيُمْسِكْ عن شَعْرِهِ وَأَظْفَاره

((Pindi mkiona mwandamo wa mwezi wa Dhul-Hijjah na mmojawenu akitaka kuchinja, basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake))

 

Na lafdhi ya Abuu Daawuuwd, Muslim na An-Nasaaiy:

 

مَنْ كَانَ لَهُ ذَبْحٌ يَذْبَحُهُ فَإِذَا أَهَلَّ هِلالَ ذِي الْحِجَّةِ فَلا يَأْخُذَنَّ مِنْ شَعْرِهِ وَلا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا حَتَّى يُضَحِّيَ  

 

((Ikiwa kuna mwenye mnyama wa kuchinja, basi utakapoandama mwezi wa Dhul-Hijjah asitoe (asikate) katu chochote katika nywele zake au kucha zake mpaka achinje))

 

Basi lafdhi hii ni dalili kwamba makatazo ya kukata nywele na kucha utakapoingia mwezi wa Dhul-Hijjah ni kwa ajili ya mwenye kutaka kuchinja pekee.

 

Riwaayah ya kwanza ina amri na kuacha, na asili yake inalazimisha uwajibu. Wala hatujui kinachohamisha hilo na asili hii.

 

Ama Riwaayah ya pili kuna katazo la kuchukua (kukata, kuondosha), na asili yake ni kulazimu uharamu; yaani uharamu wa kuondosha (kukata). Na hatujui chenye kugeuza kinachogeuza kutoka katika hilo (haramisho).

 

Hivyo imebainika kwamba Hadiyth ni makhsusi kwa mwenye kutaka kuchinja pekee.

 

Ama anayechinjiwa kwa ajili yake, ikiwa ni mkubwa au mdogo hakuna makatazo ya yeye kukata au kutoa chochote katika nywele zake au ngozi yake au kucha zake kwa kujengea juu asili yake ambayo ni kujuzu. Na hatujui dalili inayoonesha kinyume na asili yake.

 

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (11/426-427)]

 

 

Share