Imaam Ibn Baaz: Maulidi Salaf Walimpenda Zaidi Nabiy Nao Ni Wajuzi Zaidi Na Hawakusherehekea Maulidi

 

 

Salaf Walimpenda Zaidi Nabiy Nao Ni Wajuzi Zaidi Na Hawakusherehekea Maulidi.

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

“Haijuzu mikusanyiko ya Mawlid ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala mengine, kwani hayo ni katika mambo ya bid‘ah yaliyozuliwa katika dini, kwa sababu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuyafanya wala Makhalifa wake waongofu, wala wengine miongoni mwa Maswahaba wala Mataabiina walio katika karne zilizo bora; nao ni wajuzi zaidi wa Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuliko watu wengine. Nao pia ni wakamilifu wa mapenzi zaidi kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wenye kufuata Shariy’ah Yake kuliko waliokuja baada yao.” [Hukmul Ihtifaal Bilmawlid an-Nabawiy]

 

 

Share