Supu Ya Mahindi, Karoti Na Viazi

Supu Ya Mahindi, Karoti Na Viazi

Vipimo

Karoti (katakata ndogo ndogo) - 3

Viazi (katakata vidogo vidogo – cubes) - 3

Mahindi (chembe) - 2 vikombe

Mraba wa supu ya nyama au kuku - kidonge 1 (au supu yenyewe kiasi kidogo tu cha kutia ladha lakini hakikisha supu isizidishe kipimo)

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Ndimu - 1 kijiko cha chai

Siagi au mafuta - 2 vijiko vya supu

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Tia siagi au mafuta katika sufuria, kaanga viazi, vikiwa karibu na kuwiva tia karoti, endelea kukaanga kama dakika tatu hivi.
  2. Tia mahindi changanya vizuri katika moto mdogo.
  3. Tia maji kiasi, tia kidonge cha supu (Stock), tia pilipili manga, chumvi na ndimu
  4. Acha ichemke hadi viazi na karoti ziwive vizuri.
  5. Saga nusu yake katika mashine ya kusagia (blender) urudishe ndani ya sufuria. Changanya pamoja.
  6. Mimina katika bakuli ikiwa tayari.
Share