Mikate Ya Maji Ya Vitunguu Na Kotimiri

Mikate Ya Maji Ya Vitunguu Na Kotimiri

Vipimo

Unga mweupe -  2 vikombe vikubwa

Mayai - 2

Vitunguu - 2

Kotimiri - 1 msongo (bunch)

Maziwa -  3 vijiko vya kulia

Maji - 3 Vikombe

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Samli ya kupikia     

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya maziwa ya unga katika maji kikombe kimoja. Tia yai changanya vizuri.
  2. Katika bakuli, weka unga, chumvi. Kisha changanya na maji upige kwa mchapo wa mkono. Ongezea mchanganyiko wa maziwa na yai uendelee kuchanganya.
  3. Tazama uzito wa unga, ukipenda mikate mepesi ongeza maji kidogo tu kama robo kikombe uchanganye.
  4. Katakata vitunguu slaisi kisha vichambue.
  5. Katakata kotimiri kisha changanya vyote katika unga ukoroge vizuri.
  6. Weka kikaangio kikubwa katika moto, kisha teka mteko kwa upawa wa duara utandaze mkate. Teka tena uweze kupika vijikate viwili vitatu katika kikaangio kimoja.  Kikaangio kiwe kisichongandisha (non-stick).  
  7. Acha unga ukauke upande mmoja, na uive ugeuke rangi kisha geuza upande wa pili.

 

  1. Acha uive kisha tia samli kijiko kimoja cha kulia ukaange mkate hadi uive na kugeuka rangi ya hudhurungi (golden brown)
  2. Epua ikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Kidokezo:   

Ukipenda pika katika kikaangio cha kutoa mkate mmoja. 

 

 

 

 

 

 

 

Share