Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Al-Muharram: Swiyaam Za Al-Muharaam Ni Kufunga Mwezi Mzima? Au Nitakuwa Nimezusha?

 

Swiyaam Za Al-Muharaam Ni Kufunga Mwezi Mzima? Au Nitakuwa Nimezusha?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 

Je kuna fadhila za Swiyaam mwezi mzima wa Al-Muharram? Na je nikifunga nitakuwa nimezusha?

 

 

JIBU:

 

 

Baadhi ya Fuqahaa (Wanazuoni) wamesema: Ni Sunnah kufunga mwezi mzima wa Al-Muharram. Wanatoa dalili ya kauli yake Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) “Swawm bora kabisa baada ya Ramadhwaan ni Swawm ya mwezi Mtukufu wa Allaah (mwezi wa) Al-Muharram" [Muslim 1163]

 

Hata hivyo haijathibiti kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alifunga mwezi wote, na mwezi aliokuwa akifunga sana baada ya mwezi wa Ramadhwaan ni mwezi wa Sha'baan kama ilivyo kwenye Hadiyth Swahiyh kutoka ‘Aaishah (Radhwiya-Allaahu ‘anhaa):    "Sijamuona akifunga zaidi kama alivyokuwa akifunga Sha'baan." [Swahiyh Al-Bukhaariy 1969].

 

Hata hivyo haisemwi kwa yule aliyechagua kufunga mwezi mzima kuwa ni mzushi, kwa sababu Hadiyth iliyotajwa inaweza kuwa na maana hii, yaani kufunga mwezi wote kama walivyotaja baadhi ya Fuqahaa.   

 

[Majmuw’ Fataawaa Wa Rasaail Ash-Shaykh Muhammad Swaalih Al-‘Uthyamiyn Mjalada 20 Kitaab Asw-Swiyaam]

 

 

 

Share