Saladi Ya Kabeji Na Karoti

Saladi Ya Kabeji Na Karoti

Vipimo

Kabeji - 1/2

Karoti - 2

Tango - 1

Namna ya Kutayarisha

  1. Kata kabeji nyembamba sana
  2. Zikune  karoti zitoke nyembamba
  3. Kata tango vipande vidogo vidogo.
  4. Kisha changanya pamoja tia kwenye bakuli

UKWAJU

Vipimo

Ukwaju - 1 paketi moja (gm 100)

Maji - 2 vikombe

Kitunguu saumu(thomu/galic) - chembe tatu

Tangawizi - kipande kidogo tu

Tende - 3

Kitunguu maji - 1 kidogo

Nyanya - 1 ndogo

Pili pili mbichi - 3

Namna ya Kutayarisha

  1. Toa kokwa katika ukwaju
  2. Rowanisha na maji kisha kamua na utupe kokwa
  3. Tia katika sufuria na tia vitu vyote vingine ndani ya sufuria.Chemsha, na ikianza kuchemka ipike kwa muda wa dakika 5.
  4. Epua na uache upoe kisha usage katika mashine ya kusagia (blender) – uko tayari kuliwa na kuku na saladi. 

 

 

 

 

Share