Saladi Ya Makaroni Mayai Ya Kuchemsha Na Zaytuni

Saladi Ya Makaroni Mayai Ya Kuchemsha Na Zaytuni

Vipimo:

Pasta (macaroni madogo dogo) - 300 gms

Mayai ya kuchemshwa - 3

Pilipili boga (capsicum) - ½ kila

Kitunguu au kitunguu mwitu (spring onions) - 1

Zaytuni nyeusi  (olives) - ½ kikombe

Tango katakata - 1

Karoti katakata nyembamba ndefu - 1

Mahindi yaliyochemshwa - ½ kikombe

Sosi ya saladi (salad dressing)

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

 1. Chemsha mayai yawive vizuri sana. Menya katakata vipandevipande kiasi.

 2. Katakakata pilipili boga vipande kiasi vidogodogo

 3. Chemsha macaroni yaive kiasi yasilainike sana, yaani yawe magumu kiasi.

 4. Chuja maji, weka macaroni katika friji yapoe.

 5. Katika bakuli la saladi kubwa, weka kila kitu changanya vizuri.

 6. Wakati wa kupakua, nyunyizia salad dressing uchanganye vizuri tena.

 7. Onja chumvi, ongeza pilipili ukipenda.

Namna ya kutengeneza salad dressing.

 1. Weka mafuta ya zaytuni kiasi ½ kikombe katika kibakuli.

 2. Tia kitunguu thomu ulosaga, tia pilipili ya unga, tia herbs mbali mbali kavu zilovurugwa kama kotmiri mwitu (parsley), zaatari (thyme), nanaa (mint leaves).

 3. Tia siki au ndimu kiasi vijiko 2 vya kulia

 4. Chaganya vizuri.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika) 

Kidokezo:  Dressing ya saladi nyengine zinapatikana tayari madukani.

 

 

 

 

 

Share